Waulize Tanzania Commission for Universities (TCU) ndiyo wanapitisha hizo programs. Inawezekana ikawa ni tofauti kati ya structure za courses, umahili wa waalimu na viwango vinavyotakiwa na Chuo husika. Digrii ya sheria ya Havard siyo sawa na digrii ya sheria ya vyuo vikuu vingine vya Marekani ingawa zote ni za sheria. Mwanasheria kutoka Havard, Yale au Princeton Universities anachukuliwa kuwa na viwango vya juu kuliko aliyetoka vyuo vingine.