Whatsapp Business: Njia mpya kutangaza biashara.

Wick

JF-Expert Member
Joined
Dec 19, 2012
Posts
8,313
Reaction score
12,170
Habari wakukaya!.
Niliamua kuiupdate whatsapp yangu nikakutana na application ya whatsapp business hii application nilianza isikia muda wakati ilipokuwa kwenye beta stage lakini sikuifatilia mpaka hivi nilipokuja ona tayari ipo kazini.
Kifupi application hii ipo kama whatsapp lakini ikiwa imetengenezwa kwa ajili ya wafanyabiashara maana imewekewa option za;
  • inatumika ndani ya simu moja na whatsapp ya kawaida
  • kuweka jina la kampuni
  • taarifa ya biashara yako
  • sehemu biashara ilipo(google map)
  • option ya kuweka shortcut message kwa wateja wako
  • ujumbe wa kuwajibu wateja wako unapokuwa haupo online
  • kuwapanga wateja wako kimtindo wa mteja mpya, ambaye hajalipwa, aliyelipwa, aliyeweka oda n.k
  • Taarifa muhimu za bidhaa zako
  • option ya kutumia namba yako ya ofisini/mezani.
  • kumbuka ni secured kama ilivyo whatsapp (end-to-end encryption)
Haya wafanyabiashara wenzangu badala ya kutumia namba yako ya kawaida umeletewa whatsapp business
ina maana ndani ya simu yako unakuwa na whatsapp mbili moja ya matumizi yako nyingine ya biashara zako!. Ondoka na whatsapp hosts zingine ambazo hazipo secured!!

Kuipakua unaweza ipata Google playstore kama Whatsapp Business au pakua hapa whatsapp business
 
Mkuu hii nimeona ni kwa watumiaji wa android pekee vipi watumiaji wa IOS
 
Mkuu hii nimeona ni kwa watumiaji wa android pekee vipi watumiaji wa IOS
me natumia android labda ujaribu tafuta apple store kama ipo!..lakini ni nzuri sanaa
 
Ngoja niidownload nione ufanisi wake.
 
Siku ya 3 naitumia. Ni nzuri sana.
 
Kuna Telegram X. Nayo ni improved version ya Telegram ya kawaida.
 
Ivi ipo kwa ajili ya kila MTU au ni special kwa watu fulan ? tangazo LA biashara unalipia au bure
 
Ivi ipo kwa ajili ya kila MTU au ni special kwa watu fulan ? tangazo LA biashara unalipia au bure
kama unasoma secondary malizana na ndalichako kwanza!...kwa wafanyabiashara wataelewa!.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…