WhatsApp Imefanya maboresho Sehemu ya Backup

WhatsApp Imefanya maboresho Sehemu ya Backup

Kasomi

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2014
Posts
11,030
Reaction score
20,391
c8d76d845753ba67bcb81f1841694120.png
Mfumo wa End-to-end encryption unazuia WhatsApp, mitandao ya simu na kampuni za Internet kuona kinachoendelea katika mazungumzo, messages na files. Lakini hapo mwanzo mfumo huo ulikwepo katika chats na calls za WhatsApp tu. Wahuni na hackers wakitaka kuchunguza chats zako walikuwa wanatafuta file la backup kwa sababu hilo file sio encrypted.

Hivi karibuni WhatsApp imeweka uwezo wa encryption katika file la backup. Hapo mwanzo ilikuwa sio salama kwa sababu file la Backup linaweza kutumika kugundua chats zako zote, Apple, Google au mtu akipata file la backup walikuwa na uwezo wa kuona chats zilizohifadhiwa katika chats za Backup.

🟢 𝗜𝗹𝗶 𝗸𝘂𝗯𝗼𝗿𝗲𝘀𝗵𝗮 𝘂𝘀𝗮𝗹𝗮𝗺𝗮 𝘄𝗮 𝗪𝗵𝗮𝘁𝘀𝗔𝗽𝗽 𝘆𝗮𝗸𝗼; 𝗵𝗮𝗸𝗶𝗸𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘂𝗺𝗲𝗲𝗻𝗱𝗮 𝗸𝗮𝘁𝗶𝗸𝗮 𝗦𝗲𝘁𝘁𝗶𝗻𝗴𝘀 > 𝗦𝗲𝗵𝗲𝗺𝘂 𝘆𝗮 𝗖𝗵𝗮𝘁 𝗕𝗮𝗰𝗸𝘂𝗽, 𝗸𝗶𝘀𝗵𝗮 𝘄𝗮𝘀𝗵𝗮 𝗺𝗳𝘂𝗺𝗼 𝘄𝗮 𝗘𝗻𝗰𝗿𝘆𝗽𝘁𝗶𝗼𝗻.

Baada ya kuwasha, itafanya backup upya katika mfumo mpya wa kutunza files ambao hakuna yeyote duniani ambaye ataweza kuona chats zako mpaka awe na password yako uliyoweka au Key yenye herufi na namba zenye tarakimu 64.

🔴 #Tahadhari Ukipoteza Key au Password yako utapoteza chats zako zote kwa sababu hakuna anayeweza kuona Key yako ya Encryption, hata WhatsApp yenyewe haiwezi kufahamu chats zako na kuzirudisha.
 
Sisi watumiaji wa unofficial WhatsApp inakula tu kwetu 🤣🤣
 
Back
Top Bottom