WhatsApp itaweka sehemu ya "ku-edit message"

Apollo

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2011
Posts
4,920
Reaction score
3,240
WhatsApp itaweka mabadiliko ambayo kila mtumiaji alikuwa anatamani kuona sehemu hii mpya inawekwa.

Kwa kawaida WhatsApp haina sehemu ya ku-edit message baada ya kuitumia. Mtu akikosea kuituma analazimika kuifuta message na kuandika upya. WhatsApp inafanya majaribio ya kuweka sehemu ya kurekebisha message ambayo umekosea kuituma (edit).

Sehemu hii itakwepo inapatikana kwa watumiaji wote wa iOS (iPhone) na watumiaji wa Android. Pia kwa watumiaji wa WhatsApp Beta ya kompyuta tayari kuna hii sehemu katika majaribio.


Soon watumiaji wa WhatsApp wataweza ku-hold message na kupata option ya EDIT. Endapo mtu akirekebisha message (edit); WhatsApp itakuwa inaandika muda ambao mtumaji amerekebisha message. Hivyo ile sehemu ya kuonyesha muda ambao message imetumwa, itabadilika na kuandika Edited 00:00 (itaweka muda ambao mtu amerekebisha message).


Feature hii tayari ipo kwenye iMessage na Telegram.

WhatsApp itaweka sehemu ya ku-edit message
 
Mkuu karibu tena jukwaani ulipotea kwa muda humu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…