Sam Gidori
Senior Member
- Sep 7, 2020
- 165
- 417
WhatsApp imesema inajaribu matumizi mapya ya mtandao huo utakaowawezesha watumiaji kutuma na kupokea ujumbe bila kutumia simu zao.
Kwa sasa, mtandao huo unakulazimu kuunganisha simu yako na kompyuta ili uweze kutumia huduma zake katika tovuti (web) na programu (desktop app). Mtandao huo sasa unakuruhusu kutumia huduma zake hata kama simu yako “haitakuwa na chaji.”
Mtandao huo umesema unajaribu huduma hiyo kwa watu wachache ili kuangalia namna ya kuboresha kabla ya kuitoa kwa watumiaji wake zaidi ya bilioni mbili duniani.
Msimbo fiche wa mwisho hadi mwisho (end-to-end encryption), ambayo ndio sifa kuu ya mtandao huo, utaendelea kufanya kazi bila kuathiriwa na huduma hii mpya.
Watumiaji wa WhatsApp wamekuwa wakilalamikia kukosekana kwa huduma hii katika mtandao huo kwa muda mrefu, wakati mitandao mingine shindani kama Telegram na Signal zikiwa na huduma hiyo kwa muda mrefu.
Chanzo: BBC