WhatsApp unaweza kuwa ni mtandao namba moja katika kusaidia, kufanikisha na hatimae kuleta mageuzi ya kisiasa hapa nchini

WhatsApp unaweza kuwa ni mtandao namba moja katika kusaidia, kufanikisha na hatimae kuleta mageuzi ya kisiasa hapa nchini

Salary Slip

Platinum Member
Joined
Apr 3, 2012
Posts
49,390
Reaction score
152,301
Mtandao wa WhatsApp, kupitia ma-group ya WhatsApp, umewaza kuwa ni mtandao unaowaleta na kuwaunganisha watu wengi zaidi kwa pamoja pengine kuliko mtandao mwingine wowote katika nchii hii, na hivyo kufanya taarifa zinazokuwa shared kupitia mtandao huu, kuwafikia watu wengi zaidi kuliko tunavyofikiria au tunavyodhani.

Nasema hivi kwasababu hivi sasa kuna ma-group ya WhatsApp ya kila aina: ya kifamilia, kiukoo ya mashule ambapo watu walisoma pamoja (msingi, sekondari, vyuo,n.k),ma-group ya seheme za kazi na mengineyo mengi.

Ma-group yote haya,mbali na kupashana habari nyingine, hivi sasa yanatumika ku-share habari za uchaguzi zinazoendelea na kuna uwezekana hata vyombo vya habari kama magazeti taarifa zake haziwafikii watu wengi kama ilivyo kwa kupitia mtandao huu.

Yaani taarifa ambazo chanzo chake ni tv,radio au gazeti,taarifa hiyo inaweza kuwafikia watu wengi zaidi kupitia makundi ya WhatsApp kuliko ambavyo taarifa hiyo inaweza kuwafikia watu hao moja kwa moja kutoka katika chanzo husika kwa maana ya tv,radio au gazti,n.k.

Hivyo,kwa mtazamo wangu,mtandao huu wa WhatsApp unaweza kuwa ni the most effective and most useful tool katika kufanikisha mageuzi ya kisiasa katika nchi hii pengine kuliko watu tunavyodhani au kufikiri.

Uzuri mwingine ni kuwa, smartphone hizi siku hizi ziko katika bei mbalimbali kuwezesha karibu kila mtu sasa kuzimiliki tofauti na miaka ya nyuma wakati zinaingia ambapo bei ilikuwa juu na zilikuwa chache sana mitaani.

Kwahiyo ndugu zangu,hasa wale wapenda mabadiliko,tambueni tu hawa jamaa wanaohangaika kudhitibi vyombo vya habari, wanaweza kuwa wanatwanga maji kwenye kinu bila kujijua kwani mitandao hivi sasa ndio kila kitu.

Nawapa pole sana popote walipo.
 
Wakidhani kuwa kwa kuifanya TBC kama channel ya CCM, wakidhani kuwa wame-win, kumbe wamenoa!

Naunga mkono hoja kuwa wananchi kwa mamilioni, hivi sasa wanategemea kupata habari zao kupitia mitandao ya kijamii.......

Hivyo vijarida vinavyodhibitiwa na watawala hawa wa CCM, kikiwemo kijarida maarufu sana kwa "Praise & worship for Magufuli" cha Tanzanite tutafungia maandazi
 
Ushahidi ni upi mkuu maana wengine hatuna hayo magroup hivyo hatuwezi kupata uhalisia wa hichi unachosema.
 
Inaelekea mikutano yenu mmeona mugombea havutii ana uwongo mwingi na hasira.. fahamu Watanzania wanajitambua sana.. hawawezi kusikiliza.. watu waliopitia kuwa waongo na kufuja mali za wananchi.. ukianzia wa vyeti feki.. wala rushwa.. mafisadi.. wengi ni wale walafi.. ndio wanafikiri tano nyingine hazitakuwepo.. pole yenu kubwaaa

Tatizo upinzani hamuna nondo.. zaidi ya udaku.. na kutumia maneno.. ya kisifa.. poleni sana.. mbili nane ndio itaongea.. mulio isoma namba.. sibirini kuisoma zaidi.. acheni uvivu wa kukaa vijiweni.. nyanyukeni mufanye kazi au biashara..
 
Mkuu! Utasababisha WhatsApp nayo ipigwe ban, maana bwana yule akisikia habari hizi atachafukwa na akili. Kiwango cha mfadhaiko wa akili alicho nacho kwa sasa kinamtosha, kikizidi kidogo tu itabidi aanze kuhudhuria clinic mirembe maana tofauti na hapo huko kwenye kampeni tutagombezwa na kufokewa Kama vile sisi ni watoto wake.
 
Maafisa vipenyo na maafisa kificho wamejaa tele kwenye ma group ya wasap ya vyuo, shule, makazini na mitaani. Si unajua tumewekeza heavily kwenye sector isiyozalisha iitwayo "usalama"? Resources hizi zingeelekezwa katika kuimarisha elimu ya ufundi ingeleta mapinduzi makubwa ya ajira zenye tija kwa vijana wetu na Taifa kwa ujumla
 
Magu baada ya kuondosha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, akaajiri vificho na vipenyo,

hizo hela alizodai ameziokoa Kama angeongeza mishahara na kutoa ajira asingeondoshwa madarakani na Lissu
 
Mtajua oct 28 kama whatssap ni zaidi ya chombo cha habari au ni magroup ya umbeya ufipa!
Sema mnategemea kushinda kwa goli la mkono kupitia hiyo Tume yenu inayowabeba kama ambavyo dola inawabeba.

Endeleeni kusomba watu kwa malori na kualika wasanii wawasaidie kupata watu wa kuongeza kichaa kama alivyoaema Mama Maria Nyerere.
 
Mtandao wa WhatsApp, kupitia ma-group ya WhatsApp,umewaza kuwa ni mtandao unaowaleta na kuwaunganisha watu wengi zaidi kwa pamoja pengine kuliko mtandao mwingine wowote katika nchii hii, na hivyo kufanya taarifa zinazokuwa shared kupitia mtandao huu, kuwafikia watu wengi zaidi kuliko tunavyofikiria au tunavyodhani.

Nasema hivi kwasababu hivi sasa kuna ma-group ya WhatsApp ya kila aina:ya kifamilia,kiukoo ,ya mashule ambapo watu walisoma pamoja( msingi, sekondari, vyuo,n.k),ma-group ya seheme za kazi na mengineyo mengi.

Ma-group yote haya,mbali na kupashana habari nyingine, hivi sasa yanatumika ku-share habari za uchaguzi zinazoendelea na kuna uwezekana hata vyombo vya habari kama magazeti taarifa zake haziwafikii watu wengi kama ilivyo kwa kupitia mtandao huu.

Yaani taarifa ambazo chanzo chake ni tv,radio au gazeti,taarifa hiyo inaweza kuwafikia watu wengi zaidi kupitia makundi ya WhatsApp kuliko ambavyo taarifa hiyo inaweza kuwafikia watu hao moja kwa moja kutoka katika chanzo husika kwa maana ya tv,radio au gazti,n.k.

Hivyo,kwa mtazamo wangu,mtandao huu wa WhatsApp unaweza kuwa ni the most effective and most useful tool katika kufanikisha mageuzi ya kisiasa katika nchi hii pengine kuliko watu tunavyodhani au kufikiri.

Uzuri mwingine ni kuwa, smartphone hizi siku hizi ziko katika bei mbalimbali kuwezesha karibu kila mtu sasa kuzimiliki tofauti na miaka ya nyuma wakati zinaingia ambapo bei ilikuwa juu na zilikuwa chache sana mitaani.

Kwahiyo ndugu zangu,hasa wale wapenda mabadiliko,tambueni tu hawa jamaa wanaohangaika kudhitibi vyombo vya habari, wanaweza kuwa wanatwanga maji kwenye kinu bila kujijua kwani mitandao hivi sasa ndio kila kitu.

Nawapa pole sana popote walipo.
Kumbuka nasaha hizi kutoka kwa J.k Nyerere "Umasikini, Maradhi na Ujinga" ni miongoni mwa majanga yaliyokuwa yakiwasumbua watanganyika wakati ule, Kama unathubutu kusema kuwa Kuna vyombo vya habari havitoi taarifa kikamilifu kwa kile unachodai kuwa ni pingamizi basi naweza kukuingiza kwenye kundi la watanganyika wa wakati wa enzi za J.k Nyerere.
 
Magu baada ya kuondosha wafanyakazi hewa na wenye vyeti feki, akaajiri vificho na vipenyo,

hizo hela alizodai ameziokoa Kama angeongeza mishahara na kutoa ajira asingeondoshwa madarakani na Lissu
Kwani Lissu kamtowa lini Magu kwenye Uraisi!?
 
Back
Top Bottom