wheelchairs ntazipata wapi dar?

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Posts
3,154
Reaction score
71
Wana JF natafuta wheelchairs kwa ajili ya mzee wangu.(kwa matumizi ya nyumbani)..kama kuna mtu anaweza kujua wapi zinauzwa na bei zake..anaweza kuweka hiyo duka ntawatemblea very soon..natanguliza shukrani..nimetafuta kwa muda hapa dar sijaona ..
 
any cgemist wll have it or contact lons clubs they give out free at LIONS EYE CENTRE ZANAKI STREET
 
Pole sana kwa mzee wako kupata shida ya kutembea.
 
Pole sana kwa mzee wako kupata shida ya kutembea.
Asante mkuu, ni uzee tu siyo ugonjwa ila nilikuwa nahitaji hako ka wheelchair ili aweze kuzunguka maeneo ya karibu hata kama ni kwa kusukumwa..inaongeza ladha ya maisha kuliko kukaa sehemu kutwaa...I was looking for this thing quite sometime now..bongo kubwa lakini kwa hili nimewaza mara mbili ..bado sanaaaaa!
 


Mkuu pamoja na kumpatia mzee wheelchair bado atahitaji kufanya mazoezi ya kutembea kama uwezo wa kufanya hivyo anao.
 
Mkuu pamoja na kumpatia mzee wheelchair bado atahitaji kufanya mazoezi ya kutembea kama uwezo wa kufanya hivyo anao.
asante ushauri unazingatiwa..ila ni mzee sana 100+ hivi haijulikani vizuri exact age..docta amesema..hakuna haja ya kulazimisha obvious..
 
mkuu kuna mzee wetu mmoja amefariki hivi karibuni na aaajali ;alikuwa anatumia kwa msaada zaidi wasiliana na hawa ndugu

pauline 0718 0370 685
ama 0754 587 582
 
Jaribu Medical Stores Department, zilikuwa out of stock wakaagiza, inawezekana zimefika. Bei sikumbuki , lakini ni ya kawaida. Pia jaribu kuwaona CCBRT, wanaweza kumsaidia mzee hali yake ikawa na ahueni.
 
Dear All,

Ni matumaini yangu kuwa wote mnafahamu kuwa Kampuni ya simu za mkononi ya VODACOM ilianza shughuli zake rasmi hapa nchini toka mwaka 2000. Kitu cha kusikitisha zaidi ni kuwa mpaka leo hii haijawahi kulipa Kodi ya Mapato (Corporate Tax---asilimia 30% ya faida ya mwaka).

Ombi langu kwenu na kwa Wabunge wetu ni kuwa, mtusaidie kuhakikisha kuwa kuanzia mwaka ujao wa fedha wanaanza kulipa hiyo kodi ya mapato kwa makampuni. Kwa makisikio ya kati ni kuwa kama taifa tunapoteza kama shilingi bilioni 120 kwa miezi sita tu kwa kuwaruhuusu VODACOM kutolipa kodi ya mapato. Kuna haja ya Bunge letu kufanya uchunguzi huru na kuona kiasi gani cha mapato tumepoteza kama taifa kwa uamuzi huu wenye maswali mengi bila majibu.
 

wrong place i guess,yo could start a new thread in business or politics sub-forum
 
Mara ya mwisho mimi nilinunua wheelchair pale ilipo DTV (zamani ilikuwa Odeon Cinema), opposite yake kuna duka linauza vifaa vyote ambavyo vinatumika mahospitalini k.m vitanda vya hospitali, wheelchairs, darubini etc, yaani ni vitu vingi tu. Nilinunua mwaka jana kwa bei ya Tshs.250,000, sielewi kwa sasa kama bei ni hiyo hiyo au imeshapanda. Nenda kajaribu pale. Pole sana, ni wajibu wetu kuwalea wazee wetu, hata mimi nilimnunulia mama yangu ambaye alikuwa amevunjika mguu.
 
Hii habari ya wheel chair kama hayajakufika hutakaa uelewe umuhimu wake. Kwangu mimi mpaka wiki iliyokwisha hazikuwa zinamaanisha kitu chochote kwangu. Sasa kaja mmoja wa wazazi wetu, ni uzee pia. Mzee anadunda mwaka wa 86. Kumpeleka MOI inahitajika wheelchair walau mpaka kwenye gari, ukifika pale MOI wheelchair unazokuta unatamani kama mngekuja na ya kwenu. Kama tujuavyo Mzee hawezi kufungiwa ndani muda wote, inabidi kumtoa mara moja moja.

Sasa juzi tukawa pale Mlimani City; nilijiuliza sana moyoni kwa nini sehemu kama ile hakuna wheel chairs kwa wanaotumia.

Binafsi nashukuru kwa maelekezo yote yaliyotolewa hapa ukumbini.
 
Well said..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…