Ungekuwa mganga wa kienyeji usingepata wateja maana masharti ni mengi mno kuliko dawa.
Sina nia ya kukuudhi na sio kusudio langu.
Ungepunguza masharti maana kwanza Umuri umeshasonga sana kwa upande wa mwanamke anaetamani kuanzisha familia. Pili tayari unamtoto 1, hii inawapunguza sana nguvu wanaume wengi na pia hupunguza sana utulivu ktk ndoa maana mapenzi kwa wazazi hayafi ila huzimia tu. Kigezo cha elimu ni changamoto kubwa maana wanaume wengi wenye elimu hiyo washakutana na warembo wengi mno toka wanasoma mpaka kuajiriwa, wanajiamini na mara nyingi ni wapenda vitu vipya na kuhofia macho ya maclassmet wanao au wafanyakazi wenzao kuoa mwanamke mwenye mtoto tayari.
Watoto wapekee ktk familia hudeka sana hasa wakike so wanaume huwaepuka kuepuka lawama/makelele/kero toka kwa ndugu au wazazi pindi tofauti zinapijitokeza ndani ya ndoa.
Wanawake wanye elimu yako na kazi juu huogopwa na wanaume wengi kwakuwa huwa na kiburi/jeuri/majigambo na kujisikia kwingi hasa wanapokuwa wameolewa na mwanaume asiyekuwa na elimu ya kutosha hata kama anapesa zake za kutosha.
Mwisho wa yote muomba Mungu hachoki, akichoka keshapata.