Mpendwa hili si jukwaa lake, lakini kwa ushauri, (ingawa pia muonekana na mvuto wa mtu kwenye gari unategemea macho ya mhusika mwenyewe) mi binafsi ningechagua Spacio new model kwa kuwa ina injini ndogo na pia ni VVT-i (ina matumizi mazuri ya mafuta)( injini ni 1500cc-1800cc). OPA ina engine kubwa zaidi (1800-2000cc). Na kwa muonekano, kwangu Spacio ina muundo mzuri zaidi!
Jambo la msingi ni kununua kitu ambacho roho yako inakipenda zaidi maana ninachopenda mimi sicho unachopenda wewe ila kumbuka pia na bei ya mafuta, ni vyema kununua gari yenye injini utakayoweza kuinywesha mafuta na ambayo haitakuwa mzigo kwako.