Kwa madaktari JF,
Je,mtu mwenye "white blood cells" chache mwilini na kadiri ya vipimo vya kitaalamu hana maaradhi yanayomsumbua kwa wakati huo,anapaswa afanye nini ili kuuwezesha mwili kuzizalisha kwa wingi zaidi ili ziweze kufikia viwango vya kawaida kwa mwanaume mtu mzima? Je, kuna dawa gani au vyakula gani vya kuwezesha hilo?
Kula ARV mkuu
Unamkusudia muulizaji ana HIV? Mwali unajuwa nini maana ya ARV? ARV may refer to:Kula ARV mkuu
Jamani mbona mmeniandama??? mi nimetoa shauri.
... Mkuu !
Mi tu umenikumbusha mbali hapo juu! Namkumbuka Dr wetu [ ACO]
enzi hizo tuko primary.
Ukifungua mlango tu kishaanza kuandika,ukiketi anakuuliza jina,umri,kabila,utokako... Then anakupa cheti ukachukue dawa kabla hujajieleza uumwacho.
Ajabu wenyewe tulikuwa tunampenda vile anavyovuta benchi fasta,ukifika hukai foleni muda mrefu...
Mwenyewe akawa anajiita Mzee wa SPOT DIAGNOSIS.
[ CAUTION: Simfananishi nawe,ila hilo jibu ulilolitoa kwa jamaa limenikumbusha enzi hizo za mwalimu,nimecheka hadi machozi].
Kuna white blood cells za aina nyingi, na zote zina kazi tofauti kulinda mwili na magonjwa mbali mbali (aina ya granulocytes: neutaphils, basophils, eosinophils...aina ya agranulocytes: lymphocytes, monocytes, macrophages)...na hivyo sababu inazofanya aina moja kuwa nyingi au pungufu, sio lazima ifanye hivyo kwa aina nyingine ya WBC. Ungekuwa specific umeambiwa aina gani ya WBC imepungua, au kutoa profile ya aina zi=ote za WBC zikoje...ungeweza kupatiwa ushauri mzuri zaidi. Lakini ukisema tu WBC zimepungua...ni vigumu kutua zipi na lipi lifanyike!
Asanteni nyote kwa michango yenu wakuu!
Ni kwamba mhusika alifanya "full blood picture" na hakukutwa na ugonjwa wowote,pia vipimo vya "cancer" vilionyesha "negative" ila tu wbc zilikuwa pungufu ya 4000 ila zaidi ya 3000.Daktari mpimaji aliuliza kama mhusika ametumia dawa za malaria karibuni na jibu ni hapana.Kadiri ya maelezo ya daktari mpimaji chanzo chaweza kuhusisha mambo mengi ikiwa ni pamoja na dawa alizotumia mhusika karibuni, baadhi ya "preservatives" zinazowekwa kwenye vyakula vya makopo, sumu mbali mbali zilizo ktk hewa, nk.
Ndio maana swali halikukita kwenye chanzo cha upungufu huo bali kwenye "way forward" kwa mhusika kuuwezesha mwili ku "boost" uzalishaji wa "white blood cells" wenyewe.
Pole.
Ni vizuri pia ukaweka bayana jinsi unavojisikia, mwilini una tatizo gani
Homa?
Kukonda?
Apetait mswaki?
Maumivu?
Uvimbe?
Vidonda?
Nini?
One cannot treat lab results, they treat patient!
Kumbe ulikua umesha enda kwa daktari? Umetuuliza kwa kututega au?
hongera kwa kuwa nazo chache ingawa si nzuri sana,uchache huo unaashiria hauna infections sana ila una deffciciency ya wbc,nakushauri utumie vyakula vyenye vitamibi na proteiin za kutosha na madini mbalimbali ya chumvi kama vile iron.DR.sikira(Riobizo)from muhimbili university