Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Shirika la Afya Ulimwenguni limeonya kwamba nusu ya bara Uropa itakuwa imeambukizwa kirusi cha Covid -Omicron ndani ya wiki sita hadi nane zijazo.
Dk Hans Kluge alisema "wimbi la kutokea magharibi hadi mashariki" la Omicron lilikuwa likienea katika eneo lote, juu ya kuongezeka kwa aina ya kirusi cha Delta.
Makadirio hayo yalitokana na kesi mpya milioni saba zilizoripotiwa kote Uropa katika wiki ya kwanza ya 2022.
Idadi ya maambukizo imeongezeka zaidi ya mara mbili katika kipindi cha wiki mbili.
"Leo kirusi cha Omicron iknawakilisha wimbi jipya la mawimbi kutoka magharibi hadi mashariki, linaloenea katika eneo lote juu ya kuongezeka kwa Delta ambayo nchi zote zilikuwa zikisimamia hadi mwishoni mwa 2021," Dk Kluge aliambia mkutano wa wanahabari.
Alinukuu Taasisi ya takwimu na Tathmini ya Afya yenye makao yake makuu mjini Seattle ikitabiri kwamba "zaidi ya asilimia 50 ya wakazi katika eneo hilo wataambukizwa na Omicron katika muda wa wiki sita hadi nane zijazo".
Alisema nchi za Ulaya na Asia ya Kati zimesalia chini ya "shinikizo kubwa" wakati virusi vikienea kutoka nchi za magharibi hadi Balkan.
"Jinsi kila nchi inavyojibu lazima ifahamishwe na hali yake ya magonjwa, rasilimali zilizopo, hali ya kuchukua chanjo na muktadha wa kijamii na kiuchumi", aliongeza.
Uchunguzi wa hivi majuzi unaonyesha kuwa Omicron ina uwezekano mdogo wa kuwafanya watu kuwa wagonjwa sana kuliko aina nyingine za awali za Covid.
Lakini Omicron bado inaambukiza sana na inaweza kuwaambukiza watu hata kama wamechanjwa kikamilifu.
Idadi ya rekodi ya watu wanaoipata imeacha mifumo ya afya chini ya mkazo mkubwa.
Siku ya Jumatatu, Uingereza iliripoti kesi zaidi 142,224 zilizothibitishwa za virusi hivyo na vifo 77. Hospitali kadhaa zimetangaza matukio "muhimu" kwa sababu ya kutokuwepo kwa wafanyikazi na shinikizo linalosababishwa na Covid.
Kwingineko, idadi ya wanaolazwa hospitali pia inaongezeka. Waziri wa Afya wa Ufaransa Olivier Veran alionya wiki iliyopita kwamba Januari itakuwa ngumu kwa hospitali.
Aliongeza kuwa wagonjwa wa Omicron walikuwa wakichukua vitanda "vya kawaida" hospitalini huku Delta ikiweka mkazo katika idara za ICU.
Huko Ulaya mashariki, Poland iliripoti kuwa watu 100,000 walikuwa wamekufa kutokana na virusi nchini tangu kuanza kwa janga hilo. Poland sasa ina kiwango cha sita cha vifo vya juu zaidi ulimwenguni kutokana na Covid-19, na karibu 40% ya watu wake bado hawajachanjwa.
Huko Urusi, afisa mkuu wa afya ya watumiaji Anna Popova aliambia mkutano wa kikosi kazi cha serikali cha coronavirus kwamba bila hatua ya kudhibiti kuenea kwa virusi hivyo, idadi ya kila siku ya kesi mpya za Covid huko znaweza kufikia 100,000.
Kiwango cha maambukizi ya kila siku kilikuwa kimepungua hivi karibuni kutoka kilele cha kesi 41,335 zilizorekodiwa mapema Novemba, shirika la habari la Reuters linaripoti.
Bi Popova alisema kesi 305 zinazojulikana za Omicron zimegunduliwa kufikia sasa, katika mikoa 13 ya nchi. Urusi imesajili angalau vifo 311,281 na kesi milioni 10.5 hadi sasa.
Siku ya Jumatatu, kampuni ya kutengeneza dawa ya Pfizer ilisema itaweza kuzindua toleo la chanjo yake ambayo inatoa kinga maalum dhidi ya Omicron, itakayotolewa Machi. Wataalamu wa afya wanasema bado haijabainika iwapo hii inahitajika.
BBC Swahili