Who created God? Who made him? Where did he come from?


Umeelezea vizuri!

Swali
Jee unafikiria nini juu ya utabiri wa kweli uliomo ndani ya hivo vitabu vitakatifu?
 
Umeelezea vizuri!

Swali
Jee unafikiria nini juu ya utabiri wa kweli uliomo ndani ya hivo vitabu vitakatifu?

asante,utabir sio jambo la kushangaza sana,maana hata shekhe yhy alikuwa mtabil pia,.Enzi zile za elia,aliposema atazaliwa mkomboz si kitu cha ajabu sana ilikuwa n kutokna na mateso na kukata tamaa kwa wana wa Israel,utabil mbali mbali ulifanyik na ukatimia.,hata mimi nikitabili kaba miaka flani atazaliwa mtoto wa ajabu ambaye atakuwa na sifa flan,na kwel baada ya muda akazaliwa mtoto huyo,hata kama hata kuwa na sifa zote lkini kwa kuwa kumbukumbu ya utabil wangu iliandikwa basi nitaabudiwa.

Kusema kwba Yesu atakufa nak ufufuka baada ya siku tatu,haikuwa kitu kigeni sana kwa jamii za kiyahudi na pia misri.,kama unaelimu kuhusi unajimu utajua ni lini mwez December jua linakuwa na ukungu ama giza kisha tareh 25/26,linakuwa angavu tena
 
Yatupasa kufikilia japo kdogo2
1..kama mzung alika akaunda ndege
na kama hakuna gal wala redio iliyo jiunda yenyewe
vp wewe useme hakuna alietengeneza miti
Hakil ndogo yaweza ku2saidia kujua cc 2libuniwa
nasimwingine ni MUNGU
 
Free ideas mimi nna swali mkuu na ni kama ifuatavyo ni kwa nini mimi nikiwa nimekabwa na jinamizi au nimekutana na majini nikitamka kwa jina la bwana wetu YESU mwana wa MUNGU muumba wa mbingu na dunia na vyote vilivyomo nnawezeshwa na ROHO MTAKATIFU nguvu za lucifer pamoja na vibaraka wake mmeshindwa, , majini,marohani,wachawi,mizimu,mapepo yote yanakimbia na kutoweka kabisa,sasa mkuu hapo ndipo nnapata logic kwamba MUNGU yupo, Swali linakuja ni kitu gani kinawatowesha hao majini na mapepo na lusifer wao??? zaidi ya uyu MUNGU alie tuumba
 

Na hapo nimekusoma mkuu!

Swali
Ikiwa hawa tunaowaita manabii walijitapa tu bila ya kutumwa na Mungu [coz hayupo] Kwanini mafundisho yao yanafanana?

Mfano: Yesu [myahudi] christian na Mohamad [muarabu] Muslim. Na hao watu hawakukutana na niwazi kuwa Mohamadi hakusoma popote.
 
"Matter can neither be created nor destroyed" - hivi hii "law" ya maada imetenguliwa? if Not , Mungu yupo Milele na Milele , hajaumbwa wala hawezi kuumbwa, hajajiumba.
 
1 WAKORINTHO
10.Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu. - 11 Maana ni nani katika binadamu ayajuaye mambo ya binadamu ila roho ya binadamu iliyo ndani yake? Vivyo hivyo na mambo ya Mungu hakuna ayafahamuye ila Roho wa Mungu. 12 Lakini sisi hatukuipokea roho ya dunia, bali Roho atokaye kwa Mungu, makusudi tupate kuyajua tuliyokirimiwa na Mungu. - 13 Nayo twayanena, si kwa maneno yanayofundishwa kwa hekima ya kibinadamu, bali yanayofundishwa na Roho, tukiyafasiri mambo ya rohoni kwa maneno ya rohoni. - 14 Basi mwanadamu wa tabia ya asili hayapokei mambo ya Roho wa Mungu; maana kwake huyo ni upuzi, wala hawezi kuyafahamu, kwa kuwa yatambulikana kwa jinsi ya rohoni. - 15 Lakini mtu wa rohoni huyatambua yote, wala yeye hatambuliwi na mtu. - 16 Maana, Ni nani aliyeifahamu nia ya Bwana, amwelimishe? Lakini sisi tunayo nia ya Kristo. -
 

Kufanana kwa mafundisho sio sababu kwamba walitumwa na Mungu(kama yupo).mbona hata sera zinaweza kufanan,,,
BARACK OBAMA,anaweza kuwa anatumia /ama sera zake zafanana kwa kiasi na sera za akina ABRAHAM LINCOLN ,ama za F .KENNEDY ,lakini wakati huo yeye hakuwepo kabisa na inawezekana alikuwa hata haazaliwa.,Unachotakiwa kujua ni kwambaasimulizi siku zote yapo.Mfano,mwaka 3000,akija rais Tanzania akatumia sera za ujamaa na kujitegemea watasema (watakao kuwepo)nyerere kafufuka.!,lakini je ni kwel kafufuka?,HAPANA ni kutokana na masimulizi na historia tu.,Ukitaka kujua dini ni UONGO NA ULAGHAI UNAOPITWA NA WAKATI,angalia Quran ilivobeba mambo ambayo ni mzizi na chimbuko la ukristu ila imepindisha kidogo baadhi ya vitu ili kuifannya tofaut na Bible.
 

Pia mafundiaho ya Koran na Bible yamejaa tamaduni za maisha ya watu wa mashatiki ya kati.Watu wengi hawaju kuwa zile ni sheria navkanuni za maisha ya watu wa mashariki ya kati.Ni masimulizi ya maidha na Utamaduni wao ambayo yameandikwa vitabuni.Wameyasambaza dunia nzima wakitaka kila mtu ama jamii zingine ziamini katika imani zao na miunhu yao??,We hujiulizi kwa nn iwe mashatiki ya kati tu? kwa nn sio south Africa ama America,ama canada,ama Ireland ??,kwa nn mitume n manabii wasitoke Japani?,,Ukisoma historia vizur hutakuwa na was was na mambo haya.,
Huwa nawajibu wenzako humu kwamba kama Historia ya SHAKHA ZULU,ISACC NEWTON,ALBERT STEIN,MAHTIMA GHANDI ,ingeandikwa na kupambwa vizur,Wangeabudiwa hadi leo na tungekuwa na dini inaitwa SHAKHANISM,NEWTONISM,GHANDISM,STEINSM n.k.,lakini kwa kuwa mambo yao hayak urekodiwa basi hawapati heshima kama waipatayo akina MUSA,YESU,MOHAMED,JOSHUA,IBRAHIM,ISAKA,JOCOB,na wengine kama hao ambao kimsingi hawana utofauti zaidi ya muda wa kuwepo duniani na kile walichokifanya,nikimaanisha wengine walikuwa upande wa Dini ,wengine sayansi na wengine siasa.
 
Mungu hachunguziki. Ukuu wake ni mkubwa mno kiasi cha kwamba akili zetu hazina uwezo wa kumchunguza. Tumshukuru kwa kutuumba kwa jinsi ya ajabu.
 

Sorry swali lako sikuliona kw wakati.nakujibu hapa chini


Kubanwa na majinamizi umekujuaje??,Unatofautisha vipi jinamizi na Stress za maisha? ,jinamiz n nini??,
Kuhusu kutaja jina la YESU, na kuwa salama sio kitu cha kushangaza na wala hakimaanisha kwamba MUNGU yupu wala kwamba YESU ni mungu.,
ntakupa mfano,
Kuna mwanasayansi anaitwa Doken Paul ,aliulizwa kwamba uchumguz wake na utafiti wake unatokana na nini,akajibu anamfuta Newtown,kwamba kila anapotaka kufanya jambo linalohusiana na Sayansi ama ifumbuz basi anakuwa na jina La Newton akilini na mara nyingine hulitamka kabisa,.na akasema kwa kufanya hivo huwa anapata ufumbuzi mapema na akasema kwake yeye Newton ni kama MUNGU.

Swali hapa ni je kwel Newton ni msaada kwake kufanya kile akifanyacho??,Hii tunaita MOTIVATION ya kazi,amak ujipa moyo.Anapo taja neno Newtown nakuchapa kaz kwa bidii hujikuta akifanikiwa mambo yake,na kwa kuwa asili ya viumbe ni kudhani na kukariri ama kuishi kwa kuhisi,basi anaweza akamwabudu kwa kudhani kwel anahusika moja kwa moja na uvumbuz wake .

Turudi kwenye swala lako ,Kutaja jina la YESU,wanataja wengi sana hadi wachungaji,lakini je kuna uhalisia?,Hii ni hali ambayo imezoeleka kutokana naafundisho ya kimapokeo kutoka mashariki ya kati kumuhusu mtu huyu maarufu aliyeishi miaka ya zamani.(YESU.)

Kuna kitu tunaita Psychology,ambacho kinatokea hapa wakati mfano mchungaji akimshika kichwani muumini na kumwambia shetani toka!,kwanza kabisa muumini anakuwa anaamini kwamba anamatatizo (japo kiukwel hana).,Pili anakuwa anategemea kitu flani baada ya kushikwa kichwa huku akikemewa pepo(wanavoita wenyewe ).
Kisaikolojia mtu huyu anajua kabisa kwamba nini atafanya akisja shikwa kichwa,mfano,kuanguka chini na kutapa tapa.,jiulize kwa nini asiruke juu,na kwa nini alie na asicheke,kwa nn asikae kimya badala yake anapiga kelele??, utaona kwamba ni mazoea ambayo yapo kila mahala na ni kautamaduni flani kabaya walikojiwekea watu.
Mwaka 2000 nikiwa bado primary ,Alikuja shulen mchungaji kwa ajil ya kutoa juduma kama hiyo,wanafunzi walienda wengi kasoro mimi na jamaa kama watatu tuligoma.Nilipomuuliza mmoja wa wanafunzi ambaye alipowekewa mikono aligalala chini,akasema alifanya kama kaka yake alivofanya lakini hakukuwa na chochote kilichompelekea kufanya hivo.
Sikuridhika,miaka sita baadae mmama mmoja wam taani aliombewa nyumbani kwake akawa kama kawaida kupiga makelele na kujigalagaza chini.,Wiki moja baadae nilimuuliza tukiwa wawil jinsi ilivokuwa alinambia Alifanya vile kwa sababu pastor alimwambia nyumba yake ina matatizo!,so asingefanya vile angemdhalilisha pastor,lakini alikir kwamba hakuhisi chochote na aliambilia kuchubuka mikono na magoti,.


Jaribu ,hii muwekee mikono mtu huku ukiwa hutoi sauti na moyoni ukitaja jina lako la mwisho ama la kwanza,automatically yule mtu atafanya kama wengine.
cku hizi wachungaji wanaenda mbali hadi kuwanunu watu ili waka Act mbele za watu ili wapate waumini,ikibuma tunaskiaga wanarumbana. kuhusu malipo.


uliza kingine.....
 

Umejibu kwa siasa nyingi

Jinamiz linaweza kua mzimu,mchawi,jini ampapo likija linakupumbaza akili na kukunyima pumzi kwa lengo la kukufanya msukule au kwa manufaa yao wachawi na kazi zao

Ukiniambia stress za maisha zinapelekea kupoteza ufaham usingizini na mtu kuona kwamba amebnwa na jinamiz kisa akili inakua imechoka ni waz unanidanganya coz ata mchana stress mtu unakua nazo tena mchana kweupe unatembea barabaran mbona isitokee umbanwa pumzi na kupumbazwa akili itokee usiku tuu tena ukiwa umelala??

Ukiniambia ukiomba kwa jina la YESU af muujiza ukatokea na mashetani kukimbia eti iyo ni psycology kutokana na mindset yangu ilivyoji tune kwamba itokee hivyo kwa jinsi nlivyodhamiria kisa nmekua motivated na jina la YESU eti kwa kunipa mfano wa jamaa aliefanya ugunduz kwa kukumbuka jina la isaac newton ni wazi ata wewe utakua unanidanganya sababu kuna watu kisaikoloji wameji tune na kuamini huku wakiwa motivated na mtu kama bill gate na hawakua matajiri,wengine wamekua influenced na mtu kama obama kwamba watakua wanasiasa wakubwa ulimwenguni ikashindikana vile vile.

Swali. Mbona yakinikaba nikimtaja KAKOBE-LUSEKELO-MAMA RWAKATARE-GWAJIMA jinamizi aliondoki ila ni kwa jina la YESU tu ndio linaindoka???

Kwa kifupi ni kwamba MUNGU huwezi kujua na kuamin kama yupo mpaka pale akili yako itakapo ishia kufikiri na jutenda jambo,sasa ukimwamini yeye akitenda lile jambo katika maisha yako ndio utaamini kama yupo au ayupo.laa sivyo mkuu umu jf tutapiga porojo mpaka tupigwe ban
 
Swali. Mbona yakinikaba nikimtaja KAKOBE-LUSEKELO-MAMA RWAKATARE-GWAJIMA jinamizi aliondoki ila ni kwa jina la YESU tu ndio linaindoka???
nakujibu...,kwa swali hapa chini..
Unajuaje kwamba jinamizi kaja na unajua kwamba kaondoka??, Wewe kama wewe ulishawahi kumwona jinamizi?,
 

Jinamizi ni hali ya kupooza kwa mwili pindi ukiwa usingizini, Ila Pepo no roho chafu zinazotafuta "vessel" ili waweze kutenda matendo waliokusudia, ambapo iyo "vessel" inaweza kuwa mwili wa mwanadamu ama mnyama. Mapepo wapo, Majini wapo, Wachawi wapo (wabaya na wazuri) na Pia Mungu yupo ambae ameumba viumbe hawa wote pamoja na sisi wanadamu.
 

so what?,mbona sikuelewi,kwa hiyo kawaumba kwa makusudi gani??
 
so what?,mbona sikuelewi,kwa hiyo kawaumba kwa makusudi gani??

sasa kama pepo wapo na huwaingia watu ambapo wenye uwezo wa kuwaondoa hao mapepo ni mashehe na wachungaji ambao wanatumia jina la Mungu kuwaondoa kwenye miili ya wanadamu. Mungu kaumba kila kitu kwa kusudio lake kwa iyo kama unahitaji kujua siri zote za umungu basi siku yako ya umauti ikifika utajua tu.,ila hakuna mwanadamu aliye hai anaejua undani wa Mungu.
 
Ni vyema kwanza tukajifunza kujitambua na chimbuko letu ndipo tuhoji chimbuko la creator wa universe na uhalali wake tukiona inafaa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…