WHO: Dozi za Corona zilizotolewa mpaka sasa nchi tajiri 44 %, mataifa maskini 0.4%

WHO: Dozi za Corona zilizotolewa mpaka sasa nchi tajiri 44 %, mataifa maskini 0.4%

Shadow7

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2020
Posts
24,606
Reaction score
39,289
Shirika la Afya Ulimwenguni WHO, limesema nchi tajiri kiviwanda za kundi la G7 zina uwezo wa kutoa dozi milioni 100 za chanjo ya Corona kwa nchi maskini mwezi Juni na Julai pekee kusaidia kufikia malengo ya utoaji chanjo duniani kote katika mkutano wao wa kilele wiki hii.

FDA documents show Pfizer COVID vaccine protects after 1 dose | CIDRAP

Mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amezihimiza nchi za G7 zizingatie usawa katika utoaji chanjo akisema kusaidiana chanjo ni muhimu kufikisha mwisho awamu ngumu ya janga la Corona.

Ghebreyesus amesema kufikia sasa asilimia 44 ya dozi zote zimetolewa katika nchi tajiri lakini asilimia 0.4 pekee zimetolewa katika mataifa maskini. Mkutano wa kilele wa matiafa ya G7 umepangwa kufanyika Cornwall, England, kuanzia Juni 11 hadi 13.
 
Hii ni habari mbaya sana kwa yale mamburula yanayotaka kizezeta zezeta tu kuwaaminisha wasiokuwa na uwezo wa kupambanua mambo kuwa chanjo ni biashara na kuwa imelenga kuzinyonya nchi zinazoendelea na hasa Tanzania.

Kweli ujinga ni mzigo.
 
Kabisa
 
Manufaa ya chanjo ni yapi? kama ukipata chanjo bado unaweza kuambukizwa/kuambukiza, kuumwa na hata kufa.
Wanasema chanjo haizuii maambukizi ila inazuia ukipata maambukizi usipate zile dalili za corona ambazo ndizo zinapelekea kifo kwahiyo wanadai inasaidia kupunguza effect za corona hence vifo.
Mimi sitaki kuchanjwa ila nasema wanachosema wao
 
Back
Top Bottom