WHO: Idadi ya wavutaji sigara yapungua ulimwenguni

WHO: Idadi ya wavutaji sigara yapungua ulimwenguni

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Shirika la afya duniani WHO, limesema idadi ya wavutaji sigara duniani imepungua kwa kasi katika miaka ya hivi karibuni. WHO imezitaka nchi kuongeza hatua zaidi za udhibiti wa kukomesha uraibu wa Tumbaku.

Katika ripoti iliyotolewa leo, WHO inasema kwa mwaka 2020 watu bilioni 1.30 walikuwa wakitumia Tumbaku duniani kote ukilinganisha na watu bilioni 1.32 miaka miwili iliyopita. Idadi hiyo inatarajiwa kushuka hadi watu bilioni 1.27 kufikia mwaka 2025.

Mkurugenzi wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema inatia moyo kuona kwamba watu wachache wanatumia Tumbaku kila mwaka.

Tumbaku inakadiriwa kuwaua zaidi ya watu milioni nane kila mwaka, wengi wao ni kutokana na matumizi ya moja kwa moja. Wengine milioni 1.2 wamekuwa si wavutaji lakini waathirika wakubwa wa moshi wa sigara.

DW Swahili
 
Kuna biashara ya watu (sport,sm) mbona wanasema tumbaku tu na sigala je si hizo hizo tumbaku.
 
Watuletee na yetu wavuta bangi.

Inshort watu waogopa kufa na corona tu 😅😂.
 
Back
Top Bottom