cheka ni mzaliwa wa kinondoni,kabla ya kujitia katika masumbwi alikuwa mcheza kandanda kama walivyo vijana wengi wa kitanzania...makazi yake ya sasa ni morogoro ambapo alitia nanga hapo alivyokuwa katika harakati za kwenda south africa kutafuta maisha ndipo ailpokutana na kocha wake almaarufu kama komandoo aliyeweza kumtia katika boxing na kuzima harakati zake za kwenda south africa,hapo morogoro kuachana na masumbwi cheka ni mfanyabiashara wa chupa za plastics......umaarufu wake katika ndondi ulikuja pale baada ya kumtwanga nguli wa masumbwi tanzania rashid ''snakeman'' matumula...ni bondia mzuri anayeweza kutumia urefu wake ana pumzi za kutosha kuliko mabondia wengi wa bongo na pia hupenda kutumia ngumi za kudokoa kuchosha wapinzani wake