Who is Said Salim Bakhresa (Azam)?

Kuna watoto vichwa vyao ni vigumu wanalazimishwa kukariri physics, biology, geography wakati wangetumia huo muda kupiga danadana, kuogelea au kufanya mazoezi ya kukimbia basi tungekuwa mbali kimichezo. na Zama naye nembo yake ingepaa kimataifa.

Correct ... 100%. Ningepata muda mwingi wa kurusha mishale mimi... we acha tu
 

Sikia nkwambie Azam ni private limited company.....its owned by the original founders wa hiyo business na all decisions are made privately by its owners.....hayo ni maamuzi yao kuweka mtoto wake kua CEO au la. all activities, decision making na ku allocate funds zao effectively ni juu yao. ITS PRIVATE !! Unlike public limited companies ambazo shares zinakua issued to tha general public kwenye stock market. Tha family is just a group of entrepreneurs teamed up together with similar aims, goal and ambition !!!
 
Hiyo picha ya hapo juu sio Bakhresa anayezungumziwa. Kwa ambao hamjawahi kuona picha yake mwenyewe ni huyu mzee mwenye miwani anaetokea kwenye picha zote hapa chini.
 
acha wivu wewe unaweza kununua embe,chungwa au embe mwaka mzima si matunda ya msimu, sasa bhakhresa anatuifadhia tunatumia msimu mzima. we pinda vya kichina tuuuuu shauri yako .muone usivyokuwa mzalendo unapenda vya kichina. kwa taarifa yako vijana kibao wamepata ajira kupitia bhakhresa moja wameajiliwa ktk viwanda vya unga wa ugali, unga wa ngano, kutengeneza mikate ,keki ice cream,wengine wapo viwanda vya juice, na wengine wanakatisha tiketi pale bandarin kwenda zanzibar.
jamani mnyonge mnyongeni but haki yake mpeni.Au kwa kuwa ni muislam, acha izo hao wachina si wanakuja na wachina wenzao vibaru .shame on u.
 
Nia yake ya kumsema vibaya bakhresa sijaielewa! Haujasikia kuwa alisaidia watu wenye njaa somalia? Uliza wahanga wa mafuriko nani alikuwa wa kwanza kutoa msaada wa maji, unga na vikorokoro vingine? Hayo ni machache yanayoweza kutoa majibu, sidhanh kama ni wakati muafaka wa kumsema mtanzania huyu.
 
Jamani mimi naona kama kuna watu wanadonge humu ndani, mzee wa watu anafanya biashara zake poa kabisa, atleast hana za kutisha
 
Baresa ni mtanzania mwenye ujasiri, msimamo na uwezo mkubwa sana wa ujasiriamali. Sijui kisomo chake wala sina haja ya kujua kwani elimu yake ni kubwa sana, ameweza kuanzishana kukuza miradi ya uzalishaji mikubwa ya kusimuliwa katika historia ya tanzania. Anatoa ajira rasmi na kwa wajasiriamali wengi sana. Anaongeza thamani ya shilingi kwa kuexport processed farmers products, tofauti na wafanya biashara wengine wanaomaliza vidola vyetu. Anaajiri wasomi wengi sana na anajua kuwatumia ndio biashara yake inakua kila siku.
Sio rahi kwa sie masikini kutazama watu wanaishi humu humu na wanaziona opportunities na na kujilimbikizia mali, na kututupia mabaki yao. Ila ndio ubepari huo, ndio wivu na hasira na chuki zinaanza hivi.
Hilo hipo tangu historia za zamani. Unahisi kunyonywa? Pole, ila ndio mfumo tulio nao
 
ila huku kenya cjawahi ona bidhaa zake mkuu au labda vipo kwenye baadhi ya miji,,
 
Kuna shule au hospitali/dispensary amejenga mahali popote Tanzania ? Au tuseme ni mradi gani wa kijamii aliowahi kuendesha au anaendesha?
 
kuna shule au hospitali/dispensary amejenga mahali popote tanzania ? Au tuseme ni mradi gani wa kijamii aliowahi kuendesha au anaendesha?

jamii za kiarabu,kihindi na kipersia hawana muda na hawataki kusaidia jamii inayowazunguka.ni wao na biashara zao tu,kiujumla hawafai,maana wapo wanaexploit tu,kama ikitokea asaidie basi atapeleka kwa waarabu wenzio.

Tunatakiwa tuwe na kiongozi awatimue kama alivyofanya iddi amini
 
ukitoa msaada sio mpaka ujitangaze.ye hatoi msaada kwa kutaka sifa ndomana humsikii sana
 
ukitoa msaada sio mpaka ujitangaze.ye hatoi msaada kwa kutaka sifa ndomana humsikii sana
Hujajibu swali. Kama unafahamu mradi wowote wa kijamii alioutekeleza tuambie sijasema yeye atuambie.
 
cHIEF OFFICERS KWENYE MAKAMPUNI YA azam NI WAZUNGU SIO WATOTO WAKE
 
Chuki, roho mbaya, tuache tupige kazi nasi tutatoka.vimaneno maneno haviishi kazi kulalamika tu.mwenzio kafanikiwa nawe pigana utoke,badala yake ohhoo sijui nini hovyooo.waaafrika ndio maana hatuendelei wala kuendelezana sababu ya chuki.tubadilike jamani
 
Its not apart of our genetic makeup to be happy for each others success, its something you have to learn" Viola Davis"
 
Mijadala ya watu weusi utaijua tu, tunapoteza muda mwingi kuzungumzia watu kuliko kujifunza kutoka kwa watu. Kwa nini tusijifunze kutoka kwao ili nasi tupige hatua manake hawakuzaliwa matajiri wameweza na watoto wao hawakuzaliwa masikini.

Mohamed Dewji ameandaliwa kuwa tajiri, Azam anaandaa watoto wake kuwa matajiri sasa nyinyi mnao taka watoto wawe mawaziri na maraisi ndio mnaoleta tabu.

Kuna wakina K. P. Shah (Sumaria Group), Subhash Patel (Motsun), Khanji wa (MAC Group), Zakharia, Fidahussein, Manji and etal mara zote mmekuwa mkiwaita mafisadi lakini kiukweli ndio wameshika uchumi wa nchi na historia za wote zinaonyesha ni wagonga nyundo tu. Hawa jamaa walikuwa nyuma ya IPP miaka ya 80, leo hii Mengi hata kama ingekuwa kuna coaster inaita matajiri wapande kutokana na fortune zao yeye hana siti.

Tujifunze kutoka kwao kwanza ili nasi tusonge manake isijekuwa tumewaachia waongoze uchumi sie tunapiga domo na kujaza thread, tunapenda ujiko wa usomi tu ndio maana maprofessor wakifutwa kazi wanasimamia vidole gumba manake hawana issue tena wanabakia na enzi za mwalimu wangeheshimiwa.

Babu zenu wako bungeni toka nchi inapata uhuru na wanakula mishahara mikubwa lakini hata kiwanda cha kutengeneza pencil hawana, sasa kama tusipochukua hatua na sisi tutakuwa hivyo hivyo manake watu wanagombania kujaza thread JF wanasahau kuzalisha kwanza, kuchuuza kunafuatia halafu huduma ndio inakuja baadae ili kurahisisha uzalishaji na ugavi/uchuuzi.

Matajiri wote wa bongo ni industrialist na hao hao ndio wako katika mabenki na usafirishaji, nyie mko wapi very unfortunately wanaasili ya kiasia.
 
Kuna shule au hospitali/dispensary amejenga mahali popote Tanzania ? Au tuseme ni mradi gani wa kijamii aliowahi kuendesha au anaendesha?

Kupunguza Umasikini wetu kwa kuongeza ajila kwa vijana , kodi kwa serikali, kuonge forex income ni mchango mkubwA sana, tungekuwa na kama bakheresa 100 hIi nchi ingekuwa tofauti
 
We mpumbavu kweli yani hujui biashara ni ujanja anzisha na we biashara ka zake uone kama utamshinda
 
Nilimuon azamani kidogo kwenye mazishi ya Mzee mmoja Ki Yemen.
Ninachojua ni kuwa alianza kwa kushona viatu katika mojawapo ya mitaa ya Dar baada ya kutoka Unguja.
Alianza na biashara ya vyakula kama hasa juice na mnakumbuka wale zamani mashine za juice na vibanda vyake.Akaingia kwenye mikate,akanunua NMC na akanza kusaga sembe na ngano.
Ni tajiri mkubwa sana kwani anamiliki kampuni ya meli na bidhaa zake zinakwenda Kongo na Burundi.
Ameajiri wataalamu toka nje na ndani na ingekuwa bora kama angeifanya biashara yake kisasa zaidi kuliko kuwa within family circles.
Hapendi popularity( kama Mengi) lakini naamini yuko affiliated na politicians wa higher cycles (behind the scene).
Kwa assets aliokuwa nazo Mengi ni cha ntoto.
 
Kwa mujibu wa mafundisho ya waislamu HALAL ni vile vyote vilivyoruhusiwa(sio lazima iwe vyakula), HARAM ni vile vyote vilivyokatazwa. Ukibandika label ya HALAL kwenye bidhaa maana yake unamuondoa mashaka yule ambaye hana uhakika na u-HALAL wa kile anachokusudia kukinunua kwa mujibu wa imani ya dini yake, lakini haina maana kwamba vile vyote visivyokuwa na lable ya HALAL basi ni HARAM, vingine HARAM na vingine si HARAM.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…