IAMswaggstatic
Member
- Apr 23, 2012
- 76
- 71
Who is the best rapper, and who is the most recognized legend kati ya Profesa Jay na Mr II/SUGU!?
.., Joseph Haule 'Profesa Jay' na Joseph Mbilinyi 'Mr II/SUGU'.., wote ni rapa wa muziki wa Hip-hop, waandishi, watunzi, waasisi wa muziki, wakongwe na wanamuziki bora sana kuwahi kutokea kwenye kizazi cha muziki wa Bongo Flava/Hip hop...
Joseph Haule' Profesa Jay' amezaliwa 29 December 1975 (ana miaka 40 sasa) huko Ruvuma, Songea, Joseph Mbilinyi 'SUGU' amezaliwa 1 May 1972 (ana miaka 44 sasa) huko Mtwara, lakini ni mwenyeji wa mkoa wa Ruvumq, Songea..
Profesa Jay kaanza kufanya muziki mwaka 1993.., SUGU kaanza kufanya muziki 1990.. (wote ni moja kati ya mizizi ya muziki wa Bongo flava)
Wote hawa sasa ni viongozi wa umma, watumishi wa watu katika siasa, Profesa Jay anaongoza jimbo la Mikumi, Morogoro, Mr II anaongoza jimbo la Mbeya-Mjini (awamu ya 2).., wote wanatoka CHADEMA
Hapo awali wote waliwahi kutumia majina kadhaa kabla ya kubadilisha na kufikia kwenye majina waliyonayo sasa.., awali SUGU aliwahi kujiita Mr II, pia aliwahi kujiita 2 Proud.., Profesa Jay aliwahi kujiita Nigga Jay..,
Inawezekana SUGU akawa ndiye msanii wa muziki wa HipHop mwenye santuri nyingi...,hafi sasa ametoa santuri takribani tisa. Santuri hizi ni kama "Ni Mimi" iliyotoka mwaka 1995, Ndani ya Bongo (1996), Niite Mr II (1998), Nje ya Bongo (1999), Millennium (2000), Muziki na Maisha (2001), Itikadi (2002), SUGU (2004), Coming of Age-Ujio Wa Umri (2006) na VETO iliyotoka mwaka 2009.
Profesa Jay ana santuri kadhaa, ukiacha ile walitoa na Hard Blasters (Funga kazi)., zake binafsi ni 'Machozi, Jasho na Damu (2001)', 'mapinduzi halisi (2003)', J.O.S.E.P.H (2006), Aluta Continua (2007)
.., wanamuziki/wanasiasa hawa kwa nyakati tofauti, wamefanikiwa kuufanya muziki wa 'kizazi kipya' upate nguvu ya kusikilizwa na rika lote nchini, wametumia nguvu, muda, akili kufikisha muziki nje ya mipaka ya nchi nyakati hizo...
.., vibao vyote walivyowahi kuandika (Profesa Jay) na (SUGU/Mr II) ni vibao vikali, vyenye ujumbe, vyenye kuburudisha na vyenye kuishi muda mrefu kuliko vibao vingi vya wasanii wa sasa... nitajarajibu kutaja vibao kadhaa... (kila moja nitajaribu kutaja vibao vyake 14)
VIBAO 14 VYA PROFESA JAY..
1.Nikusaidiaje, 2.Zali la mentari, 3.Bongo Dar es Salaam, 4.Jina langu, 5.Ndio Mzee, 6.Msinitenge, 7.Hakuna noma, 8.Niamini, 9.sauti ya ghetto, 10.chemsha bongo, 11.Kipi sijasikia, 12.Piga Makofi, 13.UNA, 15.Kikao cha dharula.
VIBAO 15 VYA SUGU.
1.Hali Halisi, 2.Haki, 3.Hold on, 4.Chini ya miaka 18, 5.Hayakuwa mapenzi, 6.Mikononi mwa polisi, 7.Kiburi, 8.Siku nikianguka, 9.Wapi tunakwenda, 10.Nje ya Bongo, 11.Mambo ya fedha, 12.Deiwaka, 13.Freedom, 14.Far Dar es Salaam, 15.Mchakamchaka.
.., unafikiri nani anaweza kuwa bora kuzidi mwenzake kati ya 'Legends' hawa wawili wa muziki nchini kwetu..!?
Martin Maranja Masese,
Mwananchi wa kawaida.