Who is the KING of Sedans?

Ni kweli mkuu Audi na VW zinafanana hata dashboard zake tofauti ikiwa ni ndogo sana
 
BMW ni king ingawaje mimi sijamuelewa sana nilifanya tafiti ndogo tuu BM used kwa SA na Mercedes mwaka zikiwa zinalingana BM inakua juu mara mbili ya Mercedes kwa matoleo haya ya 2015 kuendelea....BMW SUV ndio nawakubali sana hawa jamii ya X 5 na ndugu yake X 6 gari zipo pale...
 
Umemaliza nadhani mjadala sasa ufungwe.

 
Mercedes Benz ML unaipa nafasi gani?
 
Blaza we unaongelea vitu vya 2015 sisi bongo huku gari zetu ni zile 3 series/c-class/ za 2002 huko mkuu.
 
Kwa lugha nyepesi sana sedan ndiyo hizi waswahili tunaita tax mfano wake ni Brevis, Crown, Mark x (yaani bonet linafanana na buti )
Wakati SUV mfano wake ni vx, prado, x5 , etc
Salon cars zote wasukuma hua wanaita ni taxi.
 
Nashukuru lakin kwenye SUV bado sijakuelewa
SUV ni gari ya abiria na siyo mizigo yenye 4WD na umbo linaloiruhusu kwenda off road.

SUV huwa na nafasi kubwa kutoka aridhini mpaka body linapoanzia ukilinganisha na magari mengine. Huwa na muundo ambao mbele kabisa kuna bonet ambalo ndani yake hukaa injini kisha hufuatiwa na sehemu yenye nafasi kubwa ya kukaa abiria. Body lake hujengwa juu ya chasis japo kuna baadhi ya category body haina chasis.

Hizi gari hazina mkia kama zilivyo sedan kwahivyo siti za nyuma hukunjwa kwa ajili ya vijimizigo mfano cruiser hardtop na zingine huwa na kijinafasi kidogo kwa ajili ya tumizigo twa kawaida.

Kuna category kibao za SUV ila nakutajia mifano yake kwa ujumla tu, mifano hiyo ni
-land cruiser (gx, vx, prado )
- Nissan (patrol, safari, xtrail )
-Range rover (defender, discovery, velar )
-GMC (yukon denali )
-Lincoln navigation
-cadillac escalade
-chevrolet (trail blazer, tahoe, suburban )
-dodge (calliber, nitro )
Just to mention few mkuu, hope umepata mwanga
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…