WHO: Mwaka 2022 ulikuwa na Visa mara 2 vya Kipindupindu kuliko Mwaka 2021

WHO: Mwaka 2022 ulikuwa na Visa mara 2 vya Kipindupindu kuliko Mwaka 2021

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Ripoti ya shirika la afya ulimwenguni, WHO imesema idadi ya wagonjwa wa kipindupindu kote ulimwenguni iliongezeka mara mbili mwaka uliopita wa 2022.

Syria ni moja ya nchi zilizoathirika pakubwa na kipindupindu kutokana na mizozo na uhaba wa maji kama mtoto huyu wa nchini humo anavyoonekana akichota maji machafu kwa matumizi mbalimbali

Shirika la WHO limesema, visa 470,000 viliripotiwa mwaka wa 2022 ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na visa 220,000 vya mwaka uliopita.

Hata hivyo wataalam wa WHO wanaamini kuwa takwimu hizo bado hazijitoshelezi na katika makadirio ya awali, lilitabiri kuwepo wagonjwa milioni 1.3 hadi 4 na vifo va hadi watu 143,000 kila mwaka.

Afghanistan, Cameroon, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Malawi, Nigeria, Somalia na Syria ziliathirika zaidi katika mwaka ulioshuhudia mlipuko wa juu zaidi ya ugonjwa huo.

Milipuko ya kipindupindu inahusishwa zaidi na uhaba wa maji ya kunywa mahitaji, umaskini na migogoro, na kadiri mlipuko unavyoongezeka, ndivyo inavyozidi kuwa ngumu kudhibitiwa
 
Back
Top Bottom