WHO: Si kweli, maambukizi ya Corona Kenya hayajapungua

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Duh tuwaombee jirani zetu

======

Shirika la Afya Duniani latofautiana na Kenya kuhusu kupungua kwa maambukizi ya corona - BBC News Swahili

Taarifa ya WHO inakuja baada ya rais Uhuru Kenyatta kuwapongeza Wakenya kwa juhudi zao za kukabiliana na corona
Shirika la afya duniani WHO limetilia shaka madai ya kupungua kwa idadi ya wagonjwa wa Corona nchini Kenya katika kipindi cha wiki tatu zilizopita.

Katika taarifa yake, shirika hilo limesema kwamba kushuka kwa idadi ya wagonjwa wenye maambukizi ya corona nchini Kenya hakuoneshi picha kamili ya maambukizi nchini humo.

Taarifa hiyo inajiri baada ya rais Uhuru Kenyatta wa Kenya kupongeza juhudi za Wakenya katika makabiliano dhidi ya Covid-19 akisema kwamba taifa hilo limeanza kupunguza idadi ya maambukizi.

Rais Kenyatta alisema kwamba baada ya serikali kuweka masharti ya kukabiliana na virusi hivyo Wakenya wengi walinyimwa uhuru wao lakini juhudi hizo zimezaa matunda.

''Naamini tumepiga hatua kubwa na hiyo ndio sababu tumeanza kupunguza maambukizi. lakini ili kuweza kufanya vyema zaidi ni sharti tuwe wakweli kwasababu ukweli ni muhimu kuendelea kupiga hatua zaidi'', alisema.

Kupungua huko kunatokana na kushuka kwa maambukizi katika kaunti za Nairobi na Mombasa, ambazo zinajumuisha asilimia 64 ya wagonjwa wote wa corona nchini Kenya.

WHO ilisema nini?
Hatahivyo madai hayo ni kinyume na kinachoendelea, kwa kuwa kaunti nyengine zinakabiliwa na ongezeko la maambukizi , ilisema taarifa hiyo ambayo ilitolewa siku ya Jumatatu.

Shirika hilo limesema kwamba vipimo vya Covid 19 vinavyofanyiwa watu katika maabara vimepungua nchini Kenya.
Bodi hiyo ya afya duniani pia imekosoa mipango ya kuwapima Wakenya ikisema maeneo yanayolengwa ni yale ambayo hayana hatari ya maambukizi.

Baadhi ya maabara pia zimesema kwamba zinakabiliwa na uhaba wa vifaa vya kupima mbali na vifaa vya kukusanya sampuli.
Limesema kwamba utafutaji wa watu waliokaribiana na wale walioambukizwa umepungua katika kipindi cha hivi karibuni miongoni mwa kaunti 10 zenye maambukizi ya juu ambazo zinabeba mzigo mkubwa wa ugonjwa huo.

WHO limesema kwamba asilimia 58 ya wagonjwa hawana watu waliokaribiana nao huku watu 129 pekee waliokaribiana na wenye maambukizi wakiripotiwa kuanzia tarehe mosi Agosti hadi tarehe 23 Agosti 2020.

Katika kaunti ya Nairobi kulingana na taarifa hiyo asilimia 42 ya walioambukizwa hawana watu waliokaribiana , huku zaidi ya asilimia 90 katika kaunti ya kisumu, Machakos, Mombasa, Kajiado, Busia na Nakuru wakisubiri idadi ya watu waliokaribiana nao.

WHO liliitahadharisha Kenya dhidi kutangaza kwamba wagongwa wa Covid-19 wamepungua nchini humo.

Huku ikiwa hizi ni ishara nzuri ambazo zinaweza kutumiwa ili kuonesha kupungua kwa maambukizi, tangazo hilo linafaa kuchukuliwa na tahadhari kubwa , ilisema WHO ikiongezea kwamba kuna umuhimu wa vipimo zaidi kufanywa katika maabara mbali na kuwasaka watu waliokaribiana na walioambukizwa.

Hatahivyo akizungumza wakati wa hotuba kwa taifa kuhusu ugonjwa huo, rais Kenyatta hatahivyo aliwaonya Wakenya dhidi ya kusherehekea mapema mafanikio hayo na badala yake kuchukua tahadhari.

Alisema kwamba idadi ya maambukizi inaanza kupungua baada ya kufikia kilele chake.

Source: BBC News Swahili
 
Hayawezi pungua embu tazama hapo yaan watoto hawaendi xul kwa madai ya kuepuka mikusanyiko. Sasa hapa mnarukaa mikojo na kukanyaga VIMA
 
Wakenya sjui watamka lini
Corona ni kiinimacho

Ova
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…