WHO yaidhinisha chanjo ya Moderna kwa matumizi ya dharura

WHO yaidhinisha chanjo ya Moderna kwa matumizi ya dharura

STRUGGLE MAN

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2018
Posts
8,633
Reaction score
16,586
WHO yaidhinisha chanjo ya Moderna kwa matumizi ya dharura

Shirika la Afya Ulimwenguni, WHO, limeidhinisha kwa matumizi ya dharura chanjo dhidi ya COVID-19 ya Moderna. Chanjo hiyo ya mRNA ya Marekani inaungana na chanjo za AstraZeneca, Pfizer-BioNTech na Johnson & Johnson kupitishwa katika orodha ya chanjo zinazostahili kutumika wakati wa dharura. Kuidhinishwa kwa chanjo nyengine za China za Sinopharm na Sinovac kunatarajiwa kufanyika hivi karibuni.

WHO imesema imechelewa kuidhinisha chanjo ya Moderna kufuatia kucheleweshwa kwa utolewaji wa data kutoka kwa watengenezaji. Mkurugenzi wa kampuni ya Moderna Stephane Bancel amesema wanashiriki mazungumzo na mashirika tofauti ikiwemo COVAX akimaanisha mpango unaoungwa mkono na Umoja wa Mataifa kusambaza chanjo ya COVID 19 katika mataifa masikini ili kusaidia kulinda idadi ya watu duniani.
 
Back
Top Bottom