Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 577
- 2,595
Shirika la Afya Duniani (WHO) limemfuta kazi afisa wake na Mwanasayansi aliyeongoza uchunguzi wa chanzo cha Mlipuko wa Ugonjwa wa COVID-19 nchini China baada ya kukumbwa na kashfa ya kujihusisha na tabia chafu za Kingono.
Mwanasayansi huyo anayejulikana kama Peter Ben Embarek amekumbwa na kashfa kadhaa za kujihusisha na vitendo vya ngono vinavyokwenda kinyume na taratibu na maadili ya kazi.
Sehemu ya taarifa ya WHO inadai Peter amefutwa kazi kufuatia madai ya kashfa za mwaka 2015-17 ambazo mwenyewe alikataa kuonesha ushirikiano wakati wa uchunguzi wake.
Atakumbukwa kwa kuongoza ujumbe wa WHO nchini China ambao ulitoa majibu ya asili ya virusi vya COVID-19 kuwa vilianzia kwa popo kisha kusambaa kwa binadamu.
Chanzo: Assosiate Press