WHO yarekodi maambukizi zaidi ya 250,000 ya COVID-19 ndani ya saa 24 zilizopita

WHO yarekodi maambukizi zaidi ya 250,000 ya COVID-19 ndani ya saa 24 zilizopita

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la Afya Duniani |(WHO) limeripoti kwa siku ya pili mfululizo juu ya kuongezeka kwa maambukizi ya virusi vya corona duniani, huku jumla ya visa vya vipya ikipindukia 259,000 katika muda wa saa 24 zilizopita.

Äthiopien Addis Ababa | Medizinisches Personal (Getty Images/AFP/A. Sileshi)

Kwa mujibu wa taarifa ya kila siku ya WHO maambukizi makubwa kwa siku ya Jumamosi yamerikodiwa nchini Marekani, Brazil, India na Afrika ya Kusini.

Takwimu za siku ya Ijumaa zilionesha kulikuwa na visa vipya 237,000 huku idadi ya watu wanaokufa kwa siku kutokana na ugonjwa wa COVID-19 imepanda katika siku za karibuni ikilinganishwa na miezi wiki chache zilizopita.

Kulingana na tarakimu zilizojumuishwa na shirika la habari la Reuters visa vya virusi vya corona duniani vilipindukia milioni 14 siku ya Ijumaa na janga hilo tayari limewauwa karibu watu 600,000 katika kipindi cha miezi saba iliyopita.

Wimbi hilo la maambukizi linaashiria visa milioni vimerikodiwa chini ya saa 100 zilizopita.

Maambukizi yachachamaa Afrika Kusini
Südafrika Johannesburg Soweto | Verbot von Alkohol (picture-alliance/AP Photo/T. Hadebe)

Eneo la Soweto nchini Afrika Kusini

Afrika Kusini imekuwa moja ya mataifa matano yaliyoathiriwa zaidi na janga la virusi vya corona, katika wakati ambapo maambukizi mapya kote duniani yanaashiria maisha ya kawaida hayatorejea hivi karibuni.

Idadi ya visa vya maambukizi 350,879 vilivyothibitishwa nchini Afrika Kusini ni karibu nusu ya visa vyote vilivyorikodia barani Afrika na juhudi zake za kukabiliana na janga hilo ni ishara ya matatizo yatakayowakumba mataifa yaliyo na mifumo dhaifu ya afya barani humo.

Afrika Kusini sasa iko nyuma ya Marekani, Brazil, India na Urusi kwa idadi ya maambukizi.

"Ukweli ni kwamba raia wengi wa Afrika Kusini ni kama bata waliopumzika kwa sababu hawawezi kutii miongozo ya WHO ya kuboresha hali ya usafi na kujitenga " amesema Askofu Mkuu wa Afrika Kusini na mshindi wa tuzo ya amani ya Nobel Desmond Tutu katika taarifa iliyotolewa kwa pamoja na mkewe.

Mataifa mengine hali inatishia mashaka
Nchini Marekani, vikosi vya matabibu wa kijeshi vimepelekwa mjini Texas na California kuzisaidia hospitali zilizozidiwa na idadi kubwa ya wagonjwa.
Indien Kalkutta | Coronavirus | Protest gegen Distanz-Regeln (DW/P. Samanta)

Raia wa India wakitekeleza sharti la kujitenga
Wimbi la mamabukizi linamaanisha mamilioni ya watoto nchini Marekani hawatoweza kurejea shuleni kikamilifu wakati wa majira ya mapukutiko.

Huko India, wimbi la visa vipya 34,884 vimeripotiwa ndani ya siku moja huku seirkali za mitaa zikiendelea kurejesha vizuizi katika maeneo mahsusi ya taifa hilo lenye zaidi ya wakaazi bilioni 1.

Nchini Iran, rais wa taifa hilo ametoa tangazo la kushtua kwamba huenda raia milioni 25 wameambukiwa virusi vya corona.

Rais Hassan Rouhani amekariri utafiti mpya wa wizara ya afya ambao bado haujachapishwa hadharani.

Iran ndiyo taifa lililoathiriwa vibaya na janga la virusi vya corona katika eneo la mashariki ya kati ikiwa na visa 270,000 vilivyothibitishwa.
 
Ajabu ni kuwa kuna mijamaa ikiona habari kama hizi inakasirika kweli kweli na inaweza hata kupigana ngumi.

Jambo la kushangaza, wengine wanaposikitika wengine wana kasirika?!

Ikumbukwe kuna tofauti za wazi baina ya kusikitika na kukasirika kama ilivyo kwa kusikitika na kufurahi.

Ama kweli stajaabu ya kustajaabu lakini ya Firauni ni baba lao!
 
Sasa kuna watu wakimaliza kusoma habari hizo halafu wakiangalia Tz maisha yanaendelea tu kama kawaida basi hushikwa na hasira,wanataka tuishi kinyume na uhalisia tuwe na hofu kubwa kuliko hicho tunachokihofia.
 
Ajabu ni kuwa kuna mijamaa ikiona habari kama hizi inakasirika kweli kweli na inaweza hata kupigana ngumi.

Jambo la kushangaza, wengine wanaposikitika wengine wana kasirika?!

Ikumbukwe kuna tofauti za wazi baina ya kusikitika na kukasirika kama ilivyo kwa kusikitika na kufurahi.

Ama kweli stajaabu ya kustajaabu lakini ya Mussa ni baba lao!
Edit tafadhali panaposomeka "MUSA" pasomeke "FIRAUNI"
 
Sasa kuna watu wakimaliza kusoma habari hizo halafu wakiangalia Tz maisha yanaendelea tu kama kawaida basi hushikwa na hasira,wanataka tuishi kinyume na uhalisia tuwe na hofu kubwa kuliko hicho tunachokihofia.
Umeichukia habari huku ukitabasamu kinafiki
 
Sasa kuna watu wakimaliza kusoma habari hizo halafu wakiangalia Tz maisha yanaendelea tu kama kawaida basi hushikwa na hasira,wanataka tuishi kinyume na uhalisia tuwe na hofu kubwa kuliko hicho tunachokihofia.

Ili wapate nini nyinyi au sisi tukihofu?

Marekani, China, Russia, UK nk wote wamehimiza raia wao kuondoka.

Si nchi jirani hakuna anaye tu envy. Hivi huyo anayetuvalia hasira kwenye yasiyokuwa enviable ni nani?

Angalau mifano tahadhari.
 
Rouhani anasema, Wairan milioni 25 wameambukizwa COVID-19 huku wakitegemewa wengine milioni 30 mpaka 35 kuambikiza ndani ya miezi michache ijayo!!!

If that is true, ni idadi kubwa sana ukizingatia na population ya watu. Kwa data za hivi karibuni za population (82 Million), hiyo 25 million ni karibu robo tatu ya raia wote.
 
Ili wapate nini nyinyi au sisi tukihofu?

Marekani, China, Russia, UK nk wote wamehimiza raia wao kuondoka.

Si nchi jirani hakuna anaye tu envy. Hivi huyo anayetuvalia hasira kwenye yasiyokuwa enviable ni nani?

Angalau mifano tahadhari.
Sijui wenyewe mnajua zaidi kwanini mnataka tuishi kwa hofu hata wewe ni mmoja wapo ndio maana kutwa kufungua nyuzi kuzungumzia Tz na corona mpaka watu wamekuchoka,tulichokifanya Tz ni kuacha kuishi kwa hofu na kuendelea kuishi kama kawaida na huu ndio huo uhalisia wa hiyo corona hatujaokota miili barabarani wala hospitali kujaa wagonjwa. Sasa nyie hamtaki huu uhalisi mnataka tuishi kinyume na uhalisia.
 
Yani katika mambo yote aliyofanya Rais Magufuli mm nimeona la maana ni hili la Covid19 tu. Kuruhusu watu tuishi bila kutufungia alifanya maamuzi sahihi sana.
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Sijui wenyewe mnajua zaidi kwanini mnataka tuishi kwa hofu hata wewe ni mmoja wapo ndio maana kutwa kufungua nyuzi kuzungumzia Tz na corona mpaka watu wamekuchoka,tulichokifanya Tz ni kuacha kuishi kwa hofu na kuendelea kuishi kama kawaida na huu ndio huo uhalisia wa hiyo corona hatujaokota miili barabarani wala hospitali kujaa wagonjwa. Sasa nyie hamtaki huu uhalisi mnataka tuishi kinyume na uhalisia.

Basi kwa sababu umesema mwenyewe kuwa hujui, nichukue fursa hii tena kukufananisha kuwa ipo tofauti ya wazi baina ya kusikitika na kukasirika. Vile vile kati ya kusikitika na kufurahi.

Fahamuni kuwa habari zozote mbaya kuhusiana na ugonjwa huu zinasikitisha mno na ndiyo maana tunaandika kila taarifa zenye mafunzo zinapopatikana.

Kukasirika huambatana na matusi na kejeli. Angalia mabandiko yenye matusi na kejeli kuwatambua nani wenye hasira na mabandiko na ugonjwa huu kujiuliza ni kwa maslahi yapi?
 
Watu wanataka tuogope kinyago

Kisa wanamchukia raisi na wanapenda siasa mfu
 
Watu wanataka tuogope kinyago

Kisa wanamchukia raisi na wanapenda siasa mfu

Mkuu ugonjwa huu hauko Tanzania peke yake.

Ugonjwa huu hauna uhusiano wowote na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais wala nchi.

Kujaribu kuufikisha ugonjwa huu na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais au kama mtu ni kushindwa kujiendekeza haki wewe mwenyewe na hao wote unaowahusisha nao.
 
Watu wanataka tuogope kinyago

Kisa wanamchukia raisi na wanapenda siasa mfu

Mkuu ugonjwa huu hauko Tanzania peke yake.

Ugonjwa huu hauna uhusiano wowote na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais wala mtu.

Kujaribu kuuhusisha ugonjwa huu na Tanzania kama nchi au Magufuli kama rais au kama mtu, kwa hakika ni kushindwa kujitendea haki wewe mwenyewe na hao wote unaowahusisha nao. Yaani watu na nchi.
 
Basi kwa sababu umesema mwenyewe kuwa hujui, nichukue fursa hii tena kukufananisha kuwa ipo tofauti ya wazi baina ya kusikitika na kukasirika. Vile vile kati ya kusikitika na kufurahi.

Fahamuni kuwa habari zozote mbaya kuhusiana na ugonjwa huu zinasikitisha mno na ndiyo maana tunaandika kila taarifa zenye mafunzo zinapopatikana.

Kukasirika huambatana na matusi na kejeli. Angalia mabandiko yenye matusi na kejeli kuwatambua nani wenye hasira na mabandiko na ugonjwa huu kujiuliza ni kwa maslahi yapi?
Sasa kinachosikitisha hapa ni kipi? ni hivi watanzania kuishi maisha yetu kama kawaida bila hofu? wewe hili linakusikitisha sana na kukufanya kuanzisha nyuzi humu karibu kila siku kujaribu kuwatisha watanzania na corona?

Hao watu zako si ndio waliyosema Tz hospitali zimejaa wagonjwa wa corona hadi zimezidiwa na nyie wengine sasa hivi mnasema et watu wengi wanakufa kimya kimya na corona.

Hayo yote ni kujenga hofu tu kwa watu na hicho ndiyo mnachokitaka hamfurahishwi na huku watanzania kuishi bila hofu.
 
Back
Top Bottom