#COVID19 WHO yazitaka nchi tajiri kuachana na usambazaji chanjo za covid-19

#COVID19 WHO yazitaka nchi tajiri kuachana na usambazaji chanjo za covid-19

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Shirika la Afya Ulimwenguni - WHO limetoa wito kwa nchi tajiri kuachana na usambazaji wa chanjo za virusi vya corona kwa faida ya nchi maskini.

Akizungumza katika Mkutano wa Kilele wa Afya Duniani mjini Berlin, mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus amesema janga la corona litamalizika wakati ulimwengu utaamua kulimaliza. Amesema huku kukiwa na karibu vifo 50,000 kwa wiki, janga hilo bado lipo mbali kuisha.

Ghebreyesus amesema nchi ambazo tayari zimefikisha kiwango cha utoaji chanjo cha asilimia 40 - zikiwemo nchi zote za kundi la G20 - zinapaswa kuuwacha mpango wa Umoja wa Mataifa wa utoaji chanjo wa COVAX au mpango wa Umoja wa Afrika AVAT kuchukua usukani katika usambazaji wa chanjo. Ameonya kuwa hakuna nchi inayoweza kumaliza kivyake janga la corona ulimwenguni.

Mkutano wa Afya Duniani Mjini Berlin ulianza jana na utaendelea hadi kesho Jumanne na pia katika mfumo wa kidijitali.
 
Ngoja watetezi wa CORONA mwenyewe waje


Ila kidogokidogo tuu tutaelewana
 
Back
Top Bottom