Chukwu emeka
JF-Expert Member
- Jan 12, 2018
- 24,314
- 38,919
Comeback ya nguvu kama kawaida ya mabingwa wa muda wote Young Africans kupitia magoli ya Shaibu Ninja na Makambo the Congolese international,baada ya kuwa nyuma kwa goli moja hadi kipindi cha kwanza,Yanga waliingia kwa nguvu na kuwaadabisha vijana hao wa Mara ambao ni mara ya kwanza kwa kucheza TPL.
Kama kawaida sub 2 ya Tambwe na Buswita yaliiongezea nguvu timu ya wananchi ambao ni wapambanaji na wafia timu japokuwa timu inapitia kipindi kigumu kwa kukosa fedha na wachezaji kutolipwa mishahara.
Kocha Mwinyi Zahera ndiye ameonekana kuwa chachu ya ushindi wa Yanga na leo akionekana mchezaji mpya jukwaani toka Congo kuja kuongeza nguvu.
Kwa spirit hii,usishangae Yanga tukawa mabingwa msimu huu.
Daima mbele, nyuma ni mwiko....Yanga daima