Whozu asaini too much money zaidi ya milioni 60+

Whozu asaini too much money zaidi ya milioni 60+

ormystatus

Senior Member
Joined
Nov 3, 2019
Posts
111
Reaction score
223
Msanii wa muziki wa bongo fleva Whozuamesaini mkataba na kampuni ya entertainment iitwayo Too Much Money inayoongozwa na kaka yake Frank pamoja na Fred yenye ofisi zake jijini Guangzhou, China.

Na mkataba huo unahusisha Kusimamia kazi za Muziki, vichekesho pamoja na biashara ambazo zitahusisha jina la msanii huyo, mkataba huo mrefu ambao kwa mujibu wake amelipwa Dola za kimarekani 30,000 kama Deposit ambazo ni zaidi ya Millioni 60 za kibongo

Pia, akiwa nchini China Whozu amefanya kazi mbalimbali ikiwa kurekodi nyimbo kadhaa na maproducer wa China wenye asili ya Nigeria pamoja na kufanya video tatu nchini nchini humo.

Msanii wa bongo Fleva Whozu asaini dili ambalo litamlipa Zaidi ya MILIONI 60+

IMG_20191106_224503_969.jpeg


Chanzo: Hot News TZ
 
Naombeni kuuliza,hivyo huyu wozhu ni clown tu ana kipaji kabisa? Kama huwa simwelewagi maana mtu mwenye kipaji kamili anajulikana 'asubuhi' tu ya career yake
 
Tatizo la management na wasanii wa kibongo hawasemagi ukweli ila ngoja washindwane ndio utasikia wanasema mara hakuna kitu chochote mara msanii haingizii faida management na kwa msanii kama whozu mjanja mjanja hyo management ijue kabsa kurudisha hela ni ngumu sana sababu hana talent ya muziki na pia hata ukiangalia na kusikiliza nyimbo zake huoni kesho yake ataimba nin ni ujanja ujanja tu
 
Naombeni kuuliza,hivyo huyu wozhu ni clown tu ana kipaji kabisa? Kama huwa simwelewagi maana mtu mwenye kipaji kamili anajulikana 'asubuhi' tu ya career yake
You are right. Jamaa hana sauti ya kuimba basi tu huruma ya watanzania.
 
Back
Top Bottom