pole sana, take a break, think then urudi kwa umakini kidogo.
samahani sana wadada, unajua mimi sielewi sana mara nyingi mtu anaposema amekuwa na uhusiano na mtu kwa muda kadhaa kumbe mtu ana familia na alikuwa hajui...........
inawezekanaje unakubali kulala na mkaka hata hujui background yake? labda kama unataka ku-have fun, otherwise kama ni serious unataka kuwa na uhusiano na huyo mtu mi nadhani kabla hamjafika mbali mnaongea sana kuhusu nyie na kumzungusha kwingi kunasaidia kujua kama huyo mtu kweli hana commitment sehemu nyingine.
tatizo siku hizi mnadhani ukimzungusha sana mkaka atakimbia, kama akikimbia akimbie tu, huyo hakuwa wako, na hata akikupata kama ni mkimbiaji atakimbia tu.............. tena hiyo ndo itakuacha kwenye maumivu makali, bora hata akikimbia kabla hamjafika mbali...........................
tunatakiwa kujifunza jinsi ya kuingia kwenye mahusiano, vinginevyo tutaishia kila siku kuwalaumu hawa wakaka wakati sisi wenyewe hatujichungi.............................
umewasikia wanasema akijileta .............................., kwa hiyo wanaona kila siku kama tunajipeleka tu kwao.