Watu wanashangaza sana! Kuwa Membe hafai kuwa Rais wa Tanzania!! Sasa huyu wa sasa ana uwezo gani wa kuongoza? Nini kimebadilika hasa ndani ya miaka mitatu ya Uongozi wake? Na vipi yeye aliandaliwa na nani wakati nasikia hata kuwahi kushika nafasi ya chini ndani ya Chama hakuwahi pia, zaidi ya kuwa Mbunge wa Chama hicho!!
Maendeleo ya watu au maisha ya Watanzania wengi hasa wa chini yameimarika kwa kiwango gani? Hakuna la zaidi tu bora CCM ibadili mfumo wake wa kihafidhina wa mihula miwili, imtose Dr Magufuli miaka 5 inamtosha tu.
Hapana mkuu hapo nakupinga. Kwa kusema hivyo humtendei haki Rais wetu.
Nakubali maisha ya watu hayajabadilika sana zaidi ya kuwa watumishi wa serikali wananidhamu na kidogo hawajioni kama wao ni miungu wadogo na ofisi sio zao tena. Watu walio bahatika kuajiliwa kwenye ofisi, makampuni na mashirika ya umma walikuwa wanatumia ovyo sana nafasi na madaraka yao kwa kuwa nyanyasa watanzania wenzao.
Mfano; Nakumbuka siku za nyuma sana, dada yangu aliyekuwa anafanya kazi NPF wakati ule, alilia wiki nzima baada ya yeye kwa amri ya boss wake kumdhulumu baba wa watu mzee pension yake. Huyo mzee wakati ule, kulingana na maelezo ya dada yangu, ilikuwa apate shilingi elfu 21, kwa wakati ule ni hela nyingi sana, badala yake alipata shilingi elfu 13 tu.
Sasa kwa bahati mbaya au mzuri huyo dada yangu alimkuta huyo mzee kwenye ngazi za mlango wa kuingilia hiyo ofisi, wakati anarudi kutoka lunch mchana, machozi yakimtoka kwa kudhulumiwa hela zake ambazo mwenyewe alikwisha zipangia bajeti, labda ya kununua nyumba nakadhalika.
Dada yangu alikuwa mhasibu (book keeping). Alipo mwuuliza shida ni nini? Ndiyo akapata hiyo story. Ilimuuma sana.
Kwa hiyo mkuu kama wewe hukupata manyanyaso kama hayo kwenye serikali za awamu za nyuma basi inawezekana mwenzetu utakuwa aidha ndiyo mmojawao wa watendaji wa manyanyaso hayo au kwa uwezo na fursa uliyo kuwa nayo wakati huo, haikukubidi kuwa confronted na watumishi wa umma. Hiyo ilikuwa karibu kila sekta.
Na yeye aliwahi kusema kuwa kazi yake ni ngumu anajuta, CCM impumzishe tu Dr Magufuli.
Kwa hili hata mimi naona Rais hakustahili kusema hivyo. Kama yeye mwenyewe aliamua kuchukua form za kugombea urais hanabudi kulalamika. Kama kazi zina mhelemea basi ajiuzuru, lakini sio kuwakatisha tamaa viongozi wa kesho. Kama Pop anaweza kujiuzuru kwanini ishindikane kwa Rais?
Kwa kukupa matumaini tu mkuu, mimi binafsi nina uhakika Magufuli hakuwa chaguo la kwanza la Rais Kikwete na makada wa CCM, ila baada ya wao kuona Lowassa ameingia upinzani kwa kishindo, hapo nafikiri plan yao iliwatoka. Wakaona hatari iliyo kuwa mbele yao kama yeye angeshinda uchaguzi. Angelipiza kisasi, maana alikuwa na Bifu nao. Wangemkoma!
Katika kupiga mahesabu yao wakaona hawana budi kumteua mgombea ambaye kidogo wananchi wengi wanaimani yaye, ambaye ni Magufuli tu ili ku-neutralize hasira ambazo wananchi walizo kuwa nazo dhidi ya viongozi wa CCM.