Why Did You Stop Going To Church?

DiasporaUSA

JF-Expert Member
Joined
Aug 27, 2016
Posts
23,382
Reaction score
29,639
Wanajopo habari za jumapili, wale ndugu zetu wakristu natumaini leo mmeshiriki ibada katika maeneo mbalimbali.

Na wengine waliokuwa na mhe Rais mmeshiriki kwa kuchangia ujenzi wa msikiti of which kwenu is good.

Tuweke habari za siasa za mbelgiji na jiwe pembeni kidogooo.

Leo napenda tujadili sababu za wana kwa wale waamini wa ukristo ambao wana muda kidogo hawahudhurii makanisani. Ni nini hasa kimepelekea waache kushiriki ibada makanisa?

Mimi binafsi , samahani nitachanganya lugha kidogo.

Back in the days I Went to some church and when it was time for offering , they said "silent collection" meaning no coins just paper and I only had coins on me then they pulled out a speed point "swiping machine" and I was like Fvck this shit I'm outta here.

Kwa mantiki hiyo, Money became more important than praise, hence they didn't take poor people seriously.

My turning point was after a Fake pastor known as Gwajima mfufuaji , mfufuaji my foot, raised somebody from the dead and seeing his followers/misukule rejoicing.

 
Mimi nimepumzika kanisani sababu ya michango yaani ishakuwa too much aisee kila pumzi inayovutwa kanisani ni michango tu[emoji24]
 
humu wengi wanajidai kutojua nyumba za ibada wala kutokuzitambua..

na bahati mbaya sijawahi kuhudhuria mazishi ya mpagani japo sikosagi misiba...sanasana utasikia huyu hakuwa mshiriki..

ss sijui wanaojidai kutokuwa na dini hawakufi au labda wanatwaliwa mzimamzima

cc kiranga
 
Ni swala la muda, wanaoenda kanisani wote wana sababu zao
 
Kiukweli tukiacha unafki, kwenye nyumba za ibada siku hizi zinaendeshwa kimaslahi sana kuliko imani.

Zaman kanisa lilikuwa linasaidia sana jamii, ila siku hizi jamii inasaidia sana kanisa tena lazima.

Michango imekuwa mingi huku ikipewa sana msisitizo, na unaambiwa kima cha chini cha kuchangia.

Miaka ya nyuma nilishawahi kuona mbibi mmoja akitolewa kwenye foleni ya chakula cha msaada kilichokuwa kinatolewa na kanisa kwa wasiojiweza, kisa cha kutolewa ni kwasababu eti alikuwa anabiashara ya kupika vitumbua, kwahiyo akaonekana kuwa anajiweza ( what the hell was that?)

Wachungaji hasa haya makanisa ya kiroho wanawakaza sana mabinti na dada zetu.

Binafsi ile swala la kusema eti " Usiangalie matendo yangu, nisikilize ninachosema" ili nishinda. Mm huwa naangalia kila kitu.

Kanisani huwa naenda mara chache sana siku hizi, na huwa naenda kama vile ni routine tu, ila najiona imani yangu inapungua kila siku. Yani umeniombea, kwavile sijaanguka ndio unanisukuma? Ukanikata ngwala pia nikagoma kwenda chini, ndio ukaita wapambe wanilazimishe kwenda chini? Acha upimbi, sina mapepo.
 
[emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]aisee hatari sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…