Why does the donor community support a corrupt regime?

Did anyone read an article called why is African still poor? Nilisoma hii article kisha kuna siku nikasoma article moja katika FT nikasema kama waafrika hatutaamka tutaendelea maskini hadi kufa kwetu.

Hivi tumekaa tukajiuliza hizi $160 Million, mara $1 BN , mara $25 BN zinaenda wapi????. Chunguzeni ninawaguarantee kuwa 75% of the foreign aid goes to administration bullshit utasikia katika billioni kaja mtaalam kutoka UK. Wafanyakazi wa UN wanalipwa mishahara ya ndoto kabisa, wengine hadi wanasomesha watoto wao wote Europe na US. Zote hizo zinajumuishwa ndani ya aid mnayoletewa Tanzania. Je tunasaidiwa au wanawapa watu wao kazi na kuendeleza nchi zao kiuchumi!!!!
 
Bwana Zhule his spot on. Most of the donor money comes in thru the front door is taken out thru the back door. Research, Capacity building, workshops etc things which do not have direct impact to the man in the street. Guess what? Most of the work like research is done by the very people from donor countries thru know-whom connections. What happens thereafter? Your guess is as good as mine.
 


that is very deep and scarier!
 


hii ni kweli sana; kwani misaada kama ile aliyokuja nayo Bush asilimia kubwa ya mahitaji yake yanatakiwa kuwa sourced Marekani!
 
Somebody clever once wrote...

"Change won't come from the top. Change will come from a mobilezed grass roots"

I couldn't agree more...
 
Kwani hawa "donors" si tunawafuata sisi wenyewe au? Okay, hata kama hatuwafuati, kwa nini tusikatae hizo "donations" zao kama hazitusaidii? Najua baadhi mtakuja na kusema 'ooh ni viongozi wetu ndio wanaotulostisha'. Siku hizi viongozi wetu ndio wamekuwa kisingizio kwa kila kitu kibaya kinachotusumbua. Kila kitu 'viongozi wetu viongozi wetu'
 
Mwanakijiji Read my Mind
When I saw your posting ‘Why does the donor community support a corrupt regime?’ I felt like you read my mind. I just asked the same question on BBC’s Global Minds.
Kwanini? My research led me to discover hivi:
1. These corrupt regimes support western businesses. Mfano. Migodi yetu iko mikononi mwao.
2. Silaha. Wanauza silaha kwa nchi kama Congo kupitia sisi.
3. Tunauwa viwanda vyetu na kuuza mashirika yetu; wanashangilia. Hawatwambii, ‘Hey guys, stop selling and killing your industries.
4. Mademu na riba. Tunakopa, tunalipa na riba kubwa na mwishowe madeni yanaongezeka na tunaendelea kuwanyeyekea sababu wanatukopesha na kutupa hela.
5. Wanatutemea mate na wizarta yetu ya nje inawatetea, kwanini wasitupe aid hata kama tuko corrupt?

Kwaiyo hata kama tukiwa corrupt vipi hawajali
 
Wazungu wataendelea kutusaidia tu kwa sababu nao wana vested interest na misaada hiyo. Wazungu nao wana shida ya pesa kama sisi na wanapenda kusafiri kuja Afrika. Hivyo misaada hii ni sehemu ya ajira kwa wengi na chanzo cha mapato. Hivyo sehemu kubwa ya misaada hii inaishia kwenye "Technical assistance".

Ngoja niwapatie kisa kimoja. Kikwete alipotaka kufanya safari ya kwanza nchini Marekani baada ya kuteuliwa kwake kuwa Rais, mimi nilikuwa ni mjumbe wa kamati ya mawizara tuliopewa kuandaa presidential brief kuhusu misaada ya Serikali ya Marekani Tanzania.
Jukumu langu lilikuwa ni kujua nini michango ya Marekani katika sekta yangu ninayofanyia kazi.
Niliwasiliana na Ubalozi wa Marekani na taasisi nyingine za Marekani nikiwauliza je ni maeneo gani wanatoa support hapa na kiasi gani cha fedha zinatumika katika miradi hiyo.

Nilishangaa sana kwa hakuna taasisi yoyote iliyoweza kunipa exact figures and areas of support. Taasisi moja kubwa hapo nchini ya Marekani ilinishauri nifanye Google search hata baada ya kuwaambia kwanini nilikuwa nahitaji hizo takwimu.
Mwishoni sikupewa hizo takwimu. Ilibidi mimi nitafute hizo takwimu kwenye miradi inayofadhiliwa na Marekani niijuayo mimi.

Baadaye nilipigiwa simu na bosi mkubwa sana katika taasisi moja ya kimarekani akisema sikuwa muda mrefu wa kuziandaa, kitu ambacho hakikuwa kweli.

Hii inadhihirisha kuwa misaada mingi haifiki kwa walengwa, unakuta kiasi kikukbwa cha fedha kinarudi kilikotoka.

Wafadhili wanatuhitaji sisi kama tunavyowahitaji wao.
Hivyo wako tayari kufumbia macho baadhi ya madhambi yetu.
Naomba kuwasilisha.
 

MMK,

What you have said is 100% true.We should all know that,all the help the donor community is giving us,is in fact their investment.They say.."..There is no free lunch under this blue sky.."They are getting something out of it and that is why they cannot stop/threaten the government.All you hear is actually a media stunt,they have no intentions of pulling the plug,in actual sense!We will continue to be beggars of our own 'money' for quite a while if WE WON'T WAKE UP.WE NEED A VOICE,WE NEED PROPER ACTIONS.SAY NO TO "NDIO MZEE ERA".

Nawasilisha.
 

Magezi hata za engineering zipo, ila wakizitoa most of the time wanatafuta cheap labour.Canada kwa mfano ina shortage kubwa ya wahandisi wazawa hasa wa kufanya research. watatuchukua huko Tanzania na ahadi nyingi, ukienda kwao unafanya research kutokana na teknolojia yao, kwa malipo na mwamvuli wa scholarship.Mathalan unafanya research za roketi, NASA, mwezini, nuclear waste.Believe me nyingi ya hizi research are currently not relevant in our countries.Unarudi na PhD, nyumbani huna unachoweza kufanya uliyosoma yako juu mno, Tanzania kufika huko ni baada ya miaka 100! Kumbuka tunaishi kwa muda dunia hii, na elimu hasa ni kutatua matatizo ya wakati huo!.

So most of our engineers(most lecturers) who got scholarships have been victim of this 'PIPI AND SUGAR' as a result wakirudi inabidi watafute shotcourse za kupata kitu cha kuwaweka mjini! Believe me I am also a victim of this, sisemi kitu nisichokijua!!!

Nani mjanja aliyetoa scholarship au wewe uliyeenda kuwa cheap labour, ukawafanyia research nchi yao ikaendelea,wakakupa degree ukarudi nayo haizuki wala haiwasaidii watanzania kwa mazingira ya Tanzania!

So sad!
 
nakumbuka hii kitu iliwahi kuongelewa na Iddi Simba na itakuwepo kwenye post za zamani, kwamba misaada inatudumaza, badala ya kutujenga. Ukiangalia India na China walijifungia na matatizoyao wakitafuta njia ya kujikomboa, leo hii wamefanikiwa, hawakusubiri, cha USAID/EU/DANIDA/CIDA/SIDA/FINNIDA nk nk
Kuna Mtu hapa ameongelea kuwekeza kwenye Hesabu/Science ndipo tutakapo endelea.
 
mkuu nimesoma article moja ya mozambique inasema "do donors promote corruption? a case study of mozambique..."
ipo ggogles
 
Uchumi wowote wa nchi ukiwa na debt obligation lazima utakuwa na kazi kubwa kukua, Nchi yeyote inayosaidiwa haina influence katika global market forum na hivyo hatuna power ya kupenyeza bidhaa zetu zikapenetrate katika masoko ya kimataifa. Does this mean we should not do anything jibu no!!!

Kimsingi kwanza nadhani misaada tunaenda kuomba wenyewe na ndio maana tunanyanyasika na kuteseka kama vibaraka. Kwanza Tanzania iweke misingi ya kuondoa huu utegemezi wa milele na kupunguza kutegemea donors katika uchumi wetu hii itasaidia tuwe na bargaining power na matajiri.

Pili corruption ikiondolewa au hata kupunguzwa itachangia kwa kiwango kikubwa point ya kwanza kutekelezeka. Mazingira ambayo rais mwenyewe anakubali kuwa 20% of foreign aid inaliwa na huku waziri aliyepewa madaraka ya kusimamia misaada mh mkulo akiacknowledge eti rushwa haifi milele unadhani patakuwa na maendeleo zaidi ya usanii mtupu.

Tatu wazungu ni watu wanapenda sana kutumia dividing rule ili wawatawale. Pakiwepo na umoja na dhati hasa sidhani kama kuna mtu anaweza kuwatingisha kiberiti. But leo mafuta yamepatikana Znz (km yapo) unaona balozi wa Norway huyo znz, mara balozi wa sweden znz wakati zamani hawakuwa wakionekana jee kuna nini!!!!. Huku wanasema corruption kubwa but wanarelease misaada ya kiwango kikubwa vp hapa!!! yote hii ni dividing rule. Anajua akiwachokonoa hivi mtaingia line mtagongana wenyewe kwa wenyewe yeye anafaidika huku akiwaponda nyote majinga!!! ndio survival lakini je viongozi wetu afrika wameamka kuliona hilo au wanaweka 10% mbele.

Wenzetu waarabu wengi hawajosoma but wanaakili sana wanazithamini rasilimali zao sie tuna wasomi kibao but kila mtu anaangalia mishemishe zake tu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…