Andika kiswahili na kama ww ni mzuri basi wazungu watakutafuta wenyewe. Kama hiyo "DO" ndio unaona umeandika basi kazi bado unayo sana. Mimi sio mtaalam wa lugha au ushairi lakini sijaona cha kunivutia kwenye huo utunzi wa 'DO"
Sent using
Jamii Forums mobile app
Sawa, nimekuelewa.
Kwa upande wangu, mashairi yangu yanahitaji kidogo chemsha bongo na kutafakari kwa undani ili kupata ujumbe.
NB: Huwa naandika mashairi ya kiingereza na kiswahili pia.
Angalia hili shairi[emoji1370] nililoliandika takribani wiki 2 zilizopita;-
WARAKA WANGU MUHIMU:
"TUFANYE NINI 2020?"
Tumevuka salama 2019, ashukuriwe Mungu.
Tu wazima katika TZ yetu huru,
Kwa kweli twakiri 'Ni kwa Neema tu'.
Cha kwanza tufanye nini mwaka huu?
Mimi na wewe "Tutubu".
Mengi majanga yamewapata wenzetu,
Na sasa yamewapata wakwetu.
Ajali na mauaji twaona na kupotezea tu,
Mvua na mafuriko twaona na kusikitika tu.
Yale ya Kenya, Libya, China na Congo yasije tupata huku.
Waulize wana wa Israeli kama huamini tu.
Machozi yetu yahusike na Turejee kwa Mungu.
Cha pili tufanye nini mwaka huu sasa?
Mimi na wewe "Tu'save chakula".
Mahindi, mpunga, maharage, ngano, tu'save sana.
Bila kusahau snacks, vingine tusindike na tuweke kwenye 'ghala'.
Tusisubiri hao nzige waingie shamba,
Tusisubiri yapite yale miaka saba.
Muulize Farao na Yusufu kama huamini sasa.
Tutazamie mana na wale kunguru? Tutumie akili inavyotupasa.
Cha tatu tufanye nini mwaka huu pia?
Mimi na wewe "Tushirikiane" pia.
Katika kazi na ajira tuwe na moja nia.
Kwani wachina walitupita kwa gani gia?
Kwani wahindi wameweza kurithishana kwa gani wosia?
Wahitimu wa mara-paap! acheni kuvuta hisia,
Wazee wa shortcut hakuna Kanaani pasipo kuumia,
Waalimu na serikali waandaeni watoto kuwa job-creators wasio bandia,
Vijana tuwe na round-tables za maana na tuache kudandia,
Tuunganishe na tushirikiane maarifa, ujuzi, vipaji na pesa, kwa ubia.
Tujifunze kwa 'chungu' washirikianao kwa asilimia mia.
Laiti tungejua siri iliyopo katika umoja wa nia.
Pia, angalia hili [emoji1370]shairi nililoliandika takribani wiki 4 zilizopita;-
L'envoy: LINDI FLOODS
Once lived happily ever after,
Until came tragedy - Lindi's raptor.
Floods' works was softer,
As if the creditor met its debtor.
Homes torn down - so bitter!
Everyone's now a survivor.
One week's time revolutionized things!
Catastrophe visited Majaliwa's province.
Now Nineteen and counting, aftermath brings.
To this emergency everyone seems a novice!
16 villages and 3774 households injured with floods stings,
God knows, but this wasn't their choice.
Now they're in uncalculated shortage,
Mattresses, food, clothes - needing basic needs.
More than fifteen thousand got nothing to mortgage,
The touched are to come and add to survivors' needs,
Until now there're no measures gauge,
And yes, babies and oldies need their feeds!
Sent using
Jamii Forums mobile app