Sijui lini we will learn au lesson. Sikio la kufa....
This methali should be in Tanzanian katiba, ili kujikumbusha majukumu, responsibilities, uwajibikaji(yea, different meaning ili kujikumbusha vizuri)
Perfect say for us...
Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!
kama si hiyo misada si tutakufa njaa ?
Hatuwezi kufa njaa bali itatufanya tupate akili ya kukusanya mapato kutokana na rasilimali zetu tulizonazo. Fikiria ni matrilioni mangapi tumepoteza through dubious contracts (IPTL, Richmond, Makampuni ya Madini, Makampuni ya uwindaji, TICTS, Kiwira, Agreko, Songas, Netgroup Solution, EPA, Meremeta, Deep Green, Radar, Ndege mbovu ya rais, Ununuzi wa silaha etc). Hizi loopholes zinakuwepo kwasababu tunajua kesho tutapata misaada vinginevyo tungeweka mazingira ya kubana mianya ya rushwa na mikataba mibovu na kuwawajibisha ipasavyo wahusika.
Habari yenyewe mboni haieleweki..ipo nusu nusu tu..inaeleaelea..
Mkuu nami nipo njia panda.
Ninajiuliza kwamba je Waziri huyo wa maendeleo wa Uholanzi ana mamlaka ya kufuta misaada ambayo inapitishwa na Bunge?
Na pili je kama yeye anayo hayo mamlaka, basi uendeshaji wa serikali ya Uholanzi ni wa aina ya pekee kiasi cha waziri kufanya maamuzi makubwa kama hayo ambayo yanahusu ushirikiano wa kidiplomasia na nchi maskini ya Tanzania halafu ndio aandike barua kulitaarifu bunge?
Labda sababu zilizopelekea huyo mwekezaji "to loose his investment" zingeelezwa labda tutaweza kung'amua ukweli.
Wewe nawe Msaada unakusaidia nini? mimi naona unawapa kiburi tu viongozi kutofanya kazi zao vizuri maana wana cheap sources of fund! (bakuli). Ndio maana kiongozi anaweza kufanya sherehe kwa kufutia madeni? (shame)kama si hiyo misada si tutakufa njaa ?
misaada inawezakumfanya mtu hawe mtumwa kama anaitumia vibaya misaada hio.kama mtu unatumia misaada vizuri basi ni rahisi kujiendeleza na kupunguza mahitaji ya misaada hio.sema kwa vile viongozi wetu wanafuja misaada ndio maana wamekuwa kama watumwa.Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!
Nadhani maamuzi yalishafikiwa na baraza la mawaziri na yeye waziri alikuwa na wajibu wa kuliandikia bunge kuelezea uamuzi huo (ingawa umepitishwa na baraza lakini unaonekana kuwa ni wa waziri).Kuna vacuum kubwa sana kwenye story nzima..yaani ni balaa..Yanai waziri anajiamulia tu kukata funds? lahaula lakwata..halafu eti sababu ni kuwa Tz sio reliable partner kwa sababu kuna mjasiriamali wa huko amelizwa?
Mi naona nyotanyota tu...
Nadhani sasa viongozi wetu wata rudi kutafakari namna ya ku-contain aibu hii.Ndio maana mimi sipendi misaada! Misaada inatufanya tuwe watumwa wa wanaotupatia hiyo misaada. Hakuna uhuru wa kweli kama wewe ni tegemezi!