Wala sio tatizo! Ni hali ya kawaida kabisa kabisa kutokana na mabadiliko ya tamaduni na hali ya dunia kwa sasa
Hata hivyo kuna namna mnatakiwa kufanya kabla hamjaanza kupeana hilo tunda tamu na wakati mnaendelea kupeana bila kuwa na hatimiliki ili msijisahau
Usiseme mbona zamani iliwezekana kuoana kabla ya kufanya! Kabla ya kusema hivyo jiulize yafuatayo:-
1. Zamani hizo watu walioana wakiwa na umri gani? Mwanamke alifikisha miaka ishirini kabla hajaolewa? Wachache sana! Kwa sasa je?
2. Ni rahisi mwanamke kufika miaka 25, 28, 30+ kwa mazingira ya sasa bila kuonja utamu? Kama wapo kati ya 10 ni wangapi? Kama uliwahi kufanya na hukua umeolewa sasa hivi imekuwaje ugome?
3. Sababu nyingine ni kwamba siku hizi watu wanaanza sex mapema sana! Katoto kako darasa la tano lakini kameshajua kuvua chupi mbele ya mwanaume. Hii inawanyima confidence ya kukataa kuvua chupi kwa anayekuja na gia ya kukuoa
4. Mwisho kabisa ndoa sio kwenda kufanya sex tu! Ni zaidi ya hapo. Tambua kwamba hata msex mara ngapi, hata msisex ukambania au yeye akajizuia, kama alivutwa na sex pekee ya kufikia uamuzi wa kukuoa bado hamtafikia kilele cha utamu wa ndoa
Note: huu sio ushauri wa kwamba muanzia kuvuana kabla hamjaoana! Dini zote zinakataza ila za kuambiwa changanya na zako.