Why Magufuli administration misses the point on Government splurge

Status
Not open for further replies.
MKAPA ALIANDIKA 'APOLOGIA' AU UTETEZI WAKE ALIPOKARIBIA MWISHO WA MAISHA YAKE HAPA DUNIANI

Katika kumuenzi Hayati Benjamin William Mkapa ninaleta sehemu ya uchambuzi nilioufanya kuhusu kitabu chake cha 'My Life, My Purpose', kitabu kilichoandikwa na yeye mwenyewe Benjamin William Mkapa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (1995 - 2005)

Kwa mtazamo wangu, nimetoa sababu kadhaa zilizopelekea kuandikwa kwa kitabu hiki cha kusisimua, na huenda kwa sehemu inaweza kujibu swali la kwa nini kiandikwe kwa Lugha ya Kiingereza.

Nilipokuwa nikiendelea kukisoma nikabaini kuwa mtindo uliotumika ni ule ambao katika theologia tunauita kuwa ni 'Apologia' (Apologetics). 'Apologia' ni uandishi wa utetezi uliotumiwa sana na watetezi wa Kanisa katika Karne ya Kwanza hadi ya Tatu wakati Kanisa lilipokuwa linapita katika mateso na ulikuwa unachapishwa kwa njia ya vitabu ili wakuu na wenye mamlaka na maamuzi wasome. Mtindo huu ulitumiwa sana na wanatheologia na wanafalsafa nguli kama vile Justin Martyr, Tatian, na Tertullian.

Katika 'Apologia' yake, Mkapa alikuwa amefanikiwa kwa kiwango kikubwa katika kuweka utetezi wake juu ya mambo kadhaa ambayo alihisi kuwa alilaumiwa, alituhumiwa na kusingiziwa katika kipindi cha uongozi wake wa nchi. Baadhi ya mambo hayo ni pamoja na sakata la EPA, Mauaji ya Zanzibar (uk. 170-173), Mkopo wake kutoka Benki ya NBC uliomuwezesha kununua nyumba yake, sakata la ununuzi wa Radar (uk. 210-212), sakata la ununuzi wa nyumba ya Serikali nchini Italia na uhusika wa Profesa Mahalu (uk. 204-206), sakata la ubinafsishaji wa Mgodi wa Kiwira (uk. 201-202) na Benki ya NBC, ununuzi wa ndege ya Rais, na mengine mengi.

Bila shaka mambo hayo ambayo hayakuwa na ushahidi juu ya uhusika wake kuwa alijinufaisha binafsi, yalimuumiza sana Mkapa. Kwa kuwa mambo hayo yalisikika hata machoni pa jumuiya ya kimataifa na kwa kuwa yeye alikuwa amefanya sana kazi na jumuiya ya Kimataifa, na kwa kuwa yeye alikuwa ni mwanadiplomasia, atakuwa aliona kuwa njia nzuri ya kuweka kumbukumbu sahihi na kusafisha jina lake katika jamii ikiwemo Jumuiya ya Kimataifa ilikuwa ni kuandika Apologia kwa Lugha ya Kiingereza.

Katika kitabu chake hiki, Mkapa alieleza wazi kuwa hakuhusika katika ufisadi aliokuwa akishutumiwa nao na hakuacha kugusia kuwa huenda wasaidizi wake au watu wengine walitumia vibaya imani yake kwao na walijinufaisha wao wenyewe binafsi pasipo yeye kujua wala kuhusika. Alieleza kuwa suala la mkopo wake kutoka NBC taratibu zote zilikuwa zimefuatwa isipokuwa watesi wake walikiuka utu na maadili ili kumchafua kama ilivyokuwa katika suala la ununuzi wa nyumba ya Serikali kule Italia ambapo ilibidi yeye mwenyewe ajitokeze Mahakamani kutoa ushahidi katika kumtetea Prof. Mahalu ambaye baadaye alishinda kesi ile. Mkapa aliendelea kueleza pia kuhusu mabadiliko makubwa aliyoyafanya akiwa Rais na mchango wake mkubwa kwa Jumuiya ya Kimataifa. Hata hivyo, ingawa hakuhusika, kama Rais wa Jamhuri kwa wakati ule anakubali kuwajibika kwa mapungufu.

Pia alitumia kitabu hicho katika kushauri na kuonya mambo mengi mazito ndani ya nchi.

Alieleza kwa kina kuhusu ushiriki wake katika upatanishi na kuleta amani katika nchi za Kenya, Rwanda, Sudan, nk. Alieleza kushangazwa sana na tabia ya Watanzania kutokujali uwezo wa watu wao. Wakati yeye akisumbuliwa kwenda kutoa mada na kusaidia katika nchi za nje zikiwemo taasisi za Ulaya, Tanzania ilikuwa haimtumii sana zaidi ya kumualika kama mtu wa 'mapambo' katika dhifa mbalimbali.

*Alionyesha kutokufurahishwa sana na tabia ya baadhi ya viongozi wa sasa kujitutumua na kujimwambafai huku wengi wao wakiwa wazito kutafuta na kupokea ushauri kutoka kwa wengine. Hakufurahishwa sana pia na tabia ya viongozi wanaotoa amri zaidi kuliko majadiliano (uk. 253-254).

Mtazamo wake ulikuwa kuwa kungekuwepo chombo kingine zaidi ya Bunge ambacho kingeliundwa na watu wasomi, wastaafu (lakini sio Marais wastaafu) ambacho kingelikuwa kinapitia kwa umakini sheria zilizotungwa na Bunge kabla ya kusainiwa kuwa Sheria. Kwa mtazamo wangu, Mkapa alipendelea Bunge la Seneti kuwepo sambamba na Bunge la wawakilishi lililopo (uk. 235-236).

Alisisitiza sana kuhusu uhuru wa Mahakama na Bunge. Kwake uhuru wa vyombo vya habari unategemea sana elimu ya kutosha kwa waandishi wa habari. Hakufurahishwa sana na tabia ya viongozi wanaopenda kusifiwa tu na hawataki kukosolewa. Alijadili kwa ufasaha umuhimu wa kuwepo kwa Tume Huru ya Uchaguzi sambamba na Vyama vyote vya Siasa kufanya Siasa kwa uhuru. Alionyesha kushangazwa shule kukosa vyoo huku viongozi wakishindwa kuhamasisha wananchi kujijengea vyoo. Hakufurahishwa sana na tabia na kasumba ya utegemezi. Alionyesha kuwashangaa viongozi hasa wa Tanzania kwa kusuasua kuharakishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki huenda kwa hofu ya kupoteza vyeo na nafasi (uk.189-190).

Mkapa alionya na kuangaliza kuhusu hatari ya viongozi kupatikana au kuteuliwa kwa misingi ya ukabila, ukanda, na udini. Hakuonyesha kupendezwa na tabia ya baadhi ya viongozi kufanya mambo kwa lengo la kudhalilisha viongozi waliopita. Hakusita kumwambia ukweli Rais Chiluba wa Zambia alipokuwa akimnyanyasa Rais Mstaafu Kaunda. Mkapa alionyesha kujivunia rekodi yake ya kufufua na kuinua uchumi ikiwemo kudhibiti mfumuko wa bei wakati wa utawala wake.

Kwa ujumla, katika kitabu chake. Mkapa alionyesha kuwalenga zaidi viongozi, wasomi, na pia Jumuiya nzima ya Kimataifa ambayo ilikuwa inamfahamu na kumheshimu zaidi kwani hadi wakati anaandika kitabu, alikuwa anaitumikia kupitia makumi ya taasisi zake kama mjumbe wa bodi mbalimbali na mshauri.

Kwa mtazamo wangu, Mkapa alikuwa amefanya vizuri kufafanua mambo aliyoyaeleza katika kitabu chake.

Ninapendekeza Watanzania wote wenye elimu na dhamana ya uongozi kukisoma kitabu hiki. Viongozi wa Dini, Wahadhiri, Wafanyabiashara, Viongozi wa Taasisi, Viongozi wa Serikali, Wajasiliamali nao wakitafute na kukisoma* kitabu hiki.

Haki na uhuru wa kujieleza na kujitetea ni haki ya msingi sana katika jamii. Kwa mtazamo wangu, bila shaka Mkapa alihukumiwa mambo mengi na jamii kwa kuwa haikuwahi kumsikiliza. Kupitia kitabu hiki, sehemu muhimu ya jamii ya Watanzania na Jumuiya ya Kimataifa itapata fursa ya kufahamu alifikiri nini na kumuelewa Mkapa alikuwa ni mtu wa namna gani na hatimaye itabidi jamii irejee tena kwa upya 'hukumu' yake ya mwanzo.

Kama Mkapa alikuwa amelalamika kuwa alituhumiwa na hata kushutumiwa na kuhukumiwa na jamii pasipokusikilizwa, ni kwa kiasi gani watu wa kawaida wanaweza kuathirika? Kama mtu kama Profesa Mahalu ambaye alikuwa Balozi aliweza 'kubambikiwa' kesi ya kuliibia taifa na kumfanya Mkapa aende kutoa ushahidi Mahakamani ili kumtetea, watu wengine inakuwaje!?

Mkapa hayupo nasi sasa, lakini kazi zake, hisia zake na mawazo yake vitaendelea kuishi daima vikishuhudiwa na kitabu chake! Nilipokutana naye hivi karibuni, nilimuuliza kuhusu uwezekano wa yeye kukitafsiri kitabu hicho kwa Lugha ya Kiswahili ambapo alinipa jibu fupi sana akisema: "kinakuja"!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Mkuu Emmaus Bandekile Mwamakula - Mkuu wa Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki na Mwenyekiti Mwenza wa Umoja wa Makanisa ya Moravian ya Uamsho Duniani

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
1 Chronicles 15:1-16:36

Imitate God in work and rest

Work is one of the ways in which you imitate God. As God laboured in creation, so we are to do the same. The command to work was there before the Fall (see Genesis 2:15). As Ken Costa often says, ‘Work was in the original God-breathed prospectus.’
David set to work. He ‘constructed buildings for himself’ (1 Chronicles 15:1). He called together the leaders and set them to work (v.12).
There is no divide between the sacred and the secular. Worship was at the heart of all that they were to do. David gave instructions about ‘the work of worship’ (v.2, MSG). They were appointed ‘to minister before the ark of the Lord, to make petition, to give thanks, and to praise the Lord, the God of Israel’ (16:4). King David joined in the worship ‘dancing and celebrating’ (15:29).
At set times during the day (16:7), they took what Joyce Meyer describes as a ‘praise pause’ – ‘I do not think anything blesses God more than when we stop right in the middle of what we are doing and lift our hands to worship him… Think about a businessman, for example, maybe the president of a large company. Wouldn’t it be wonderful if several times a day, he closed the door to his office, turned the lock, knelt, and said, “God, I just want to take some time to worship you.”
‘The same is true for students, stay-at-home [parents], retired people, secretaries, flight attendees, brain surgeons, clerks, and salespeople – anyone you can think of. We all would benefit greatly from taking a “praise pause.”’
David praises and thanks the Lord for what ‘he has done’ (v.8), ‘his wonderful acts’ (v.9), ‘the wonders he has done’ (v.12). He recounts the great work of the Lord and calls the people to ‘worship the Lord in the splendour of his holiness’ (v.29).
God is a worker. We see this right from the start of the Bible. He was at work in creation, ‘by the seventh day God had finished the work he had being doing; so on the seventh day he rested’ (Genesis 2:2). He not only creates the world, he sustains and redeems it. Work really is one of the ways in which you imitate God.

Lord, thank you for work. Thank you that even ‘hard work’ is such a blessing. May my work in itself be an act of worship, as I present my body as a ‘living sacrifice… [my] spiritual act of worship’ (Romans 12:1–2).



Pippa Adds

1 Chronicles 15:29
‘As the ark of the covenant of the Lord was entering the City of David, Michal daughter of Saul watched from a window. And when she saw King David dancing and celebrating, she despised him in her heart.’
I love worship, but it is easy to have likes and dislikes. Sometimes I can think ‘how can that be worship?’ But God looks at the heart. And I don’t want to become like Michal!



Verse of the Day

‘May the favour of the Lord our God rest upon us;
establish the work of our hands for us…’ (Psalm 90:17).


Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…