Nimeitoa Group la Ccm TAIFA
Wameanza kushikana.
Hoja hujibiwa kwa hoja.....namuomba Katibu wangu Comrade Bashiru na Polepole..mnielewe...au kama mmevaa Viatu haviwatoshi semeni....mkitegemea eti Wagombea wa Upinzani wasimame kwenye Kampeni wahubiri mafanikio ya JPM kwa miaka 5..mnachemka..vibaya..
Wao kazi yao ni kupiga Spana in negative way..sio kazi yao kusifia CCM..sasa kama watasifia wanagombea ili iweje..?
Kuna hoja zinatupwa zinahitaji majibu yalionyooka...ili kuthibitisha....mafanikio
tumehubiri miaka yote 4..tumepata coverage kubwa ya Media na Magazeti..tumekwenda live on TV...mara nyingi....
Nategemea wataalamu waliokuwa wanamshauri mh Rais kufanya miradi yote wakimwambia kuwa inafaida kwa Nchi na kwa wanachi waje wajibu hoja...
Kuna hoja kuhusu Ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa CHATO....una impact gani kwa Taifa kwa sasa na kwa baadae..toka umejengwa...
Kuna hoja kuwa kwanini ATCL...imetolewa ktkt ukaguzi wa CAG..ikiwa manunuzi yake yamefuata taratibu za sheria..
Kuna hoja ya Wafanyakazi..kutokulipwa nyongeza zao kwa miaka 5..au kutokuwa na .Ajira mpya kwanini..?
Kuna hoja kwanini tunasisitiza risiti..ila Vitambulisho vya wamachinga pesa yake haina risiti inakwenda wapi..
Kuna Hoja kuwa ikiwa tunasema Serikali inapesa na miradi yote tunajenga kwa pesa zetu za ndani mpaka ndege tumenunua cash..kwa nini Deni la Taifa ndani ya mda mchache limekuwa kubwa kuliko miaka 10..ya JK. .
Kuna hoja...kwamba kwenye mikutano yenu mnalazimisha Wanafunzi na Watumishi wa Umma waende na mnawatisha...mnasomba watu na mnawapa posho..
Hizi ni Hoja zinatakiwa kujibiwa kiundani sio kusema tu wanatumwa na Mabeberu..sio Wazalendo..
Naomba Comrade Bashiru..tuweni serious Watu wa sasa wanaufahamu mkubwa...wanaona wanajua...
NB..Tuna Vijana wasomi wa UVCCM...watumieni kujibu hoja with evidence. .punguzeni mda wa Wasanii majukwaani..na sio kila kinachosemwa na wapinzani mnakijibu hata kama mlisahau kuweka kwenye Ilani
Mwisho kuna tuhuma kuwa kuwaengua wagombea wa Upinzani ni mkakati wenu CCM. .na mlifanikiwa kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa..
Hizi ni tuhuma nzito sana. .zinahitaji majibu mazuri. ..
Chief Mtemi Comrade Kiswanta [emoji120][emoji120][emoji120][emoji1756][emoji1756][emoji1756]
Sent from my SM-A715F using
JamiiForums mobile app