Why Magufuli administration misses the point on Government splurge

Status
Not open for further replies.
AINA KUU MBILI ZA WIVU:
1. WIVU WA KI-MUNGU: Ni pale unapoona mtu kafanya jambo zuri na wewe unatiwa changamoto kufanya kama vile au kwa ubora zaidi. Mtu mwenye wivu wa Ki-Mungu yupo tayari kumpongeza mwingine aliyefanikiwa bila kuwa na kinyongo moyoni. Wivu wa Ki-Mungu unawatakia wengine mafanikio na kuwawazia mawazo yaliyo mema. Mungu anajitambulisha kama "MUNGU MWENYE WIVU" (Kumb 5:9); hapendi kuona watu wake wakipotea kwa kuabudu miungu wengine. WIVU WA KI-MUNGU unatamani kwamba kila anayekuzunguka nae ainuliwe; yani isiwe ni wewe tu ndie SUPER STAR (HESABU 11:29; YOHANA 3:30-35).

2. WIVU WA KI-SHETANI: Mtu mwenye wivu huu hataki kuona mtu mwingine akifanya vizuri au akiinuka zaidi yake. Wivu wa kishetani hupelekea mtu kubuni mbinu mbalimbali za kuua au kudhoofisha vipiwa vya wengine. Mtu mwenye wivu wa Ki-Shetani yupo tayari hata kuua ili kuharibu ndoto ya mtu mwingine (MWANZO 37:20).

YAKOBO 3:16-17 (BHN); "Maana popote palipo na wivu na ubinafsi hapo pana fujo na kila aina ya uovu. 17 Lakini hekima itokayo juu mbinguni, kwanza ni safi; inapenda amani, upole na huwajali watu; imejaa huruma na huzaa matunda ya matendo mema; haina ubaguzi wala unafiki."

MUNGU ATUPONYE NA "WIVU WA KISHETANI" NA UTUPE "WIVU WA KIMUNGU," AMEN!!

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…