"Samweli akawaambia, Msiogope; ni kweli mmeutenda uovu huu wote; lakini msigeuke na kuacha kumfuata BWANA, bali mtumikieni BWANA kwa mioyo yenu yote."
Mpendwa karibu tena siku hii ili tuweze kutafakari ujumbe huu.
Pamoja na maonyo makali Samweli aliyowapa watu wake juu ya uovu waliomtenda MUNGU, bado anawakumbusha huruma ya MUNGU, kwamba wakiishi maisha ya toba ya kweli MUNGU aweza kuwakubali tena.
Uovu wako usikukatishe tamaa bado MUNGU aweza kukupokea tena, ili mradi uyaishi mapenzi yake baada ya toba.
Mpendwa unapotubu na kuishi katika kusudi la MUNGU unayaandaa maisha ya uzima wa ulimwengu ujao.
Kila wakati tambua hapa ulipo unaishi kwa kitambo kidogo,mawazo yote yawe kwenye uzima ule wa ulimwengu ujao.