Lugha gongana!
Hotuba ya leo ya Mheshimiwa Rais imeiibua mambo ya kutofautiana na Viongozi wengine ambapo sasa Sijui tufuate yapi???!!
- Waziri mkuu kasema watu tukae ndani,
Mheshimiwa Rais kasema tupige kazi.
- Naibu waziri wa Afya kasema tusifukuzie tutaunguza mfumo wa upumuaji,
Mheshimiwa Rais kasema tufukuzie kwasababu joto kali, Corona virus anakufa!
- RC Dar anasema watu wa mikoa wasije Dar, Mheshimiwa Rais kasema waje tu maana ndio sehemu kubwa ya biashara na mapato ya Nchi.
- Waziri Afya anasema waliopona 11,
Mheshimiwa Rais kasema wamepona zaidi ya 100.
- Waziri Afya anaahidi kupuliza dawa za kuulia virus (Fumigation) kupulizwa maeneo yote muhimu ya Jamii huku RC Dar akisimamia zoezi hilo kikamilifu kwa mkoa wa Dar kupuliziwa huku akimshukuru Mheshimiwa Rais kwa kuwapa dawa hizo mkoa wake,
Mheshimiwa Rais amemuagiza IGP na TAKUKURU kufanya uchunguzi kwa walioagiza kupuliza dawa hizo kwasababu ni upuuzi mtupu na Corona Virus hauawi kwa kupuliziwa dawa!
#### Hayo ni machache kati yaliyojiri kwenye hotuba yake, fikiria hali ya hao Viongozi na matamko yao siku zijazo zitakuwaje??!
Anza kufuatilia takwimu zao ukipinganisha na zilizopita!
Fuatilia pia matamko ya kitaalam kuhusiana na kujikinga na Corona virus!
Tanzania ni yetu sote 💪🏾 🇹🇿
Stay Home
Stay safe
Jikinge na ugonjwa wa COVID-19 🙏🏾