Why Tanzanian Millionaires Enrol Their Children to Kenyan Schools

Gharama za Shule nzuri Tanzania ni ghali sana, ukilinganisha na Shule ya hadhi hiyo hiyo Kenya. Mfano mzuri ni ada ya Braeburn Tanzania na Kenya
 
Hakuna mtz mjinga apeleke mtoto Kenya ache kupeleka south Africa, Zimbabwe Namibia ,Mauritius apeleke far kilometers away
Hakuna mkate mgumu mbele ya chai
 
Sioni cha ajabu ikiwa mwai kibaki mwenyewe alisoma tz
 
Yaani unaamini shule ya maana inaweza kuwa na tangazo kama hilo? Kwahiyo wanaosoma kenya ndio wakirudi bongo wanaishia kufundisha shule hizo
 
Acha uzwazwa wewe hapo tatizo ni lugha tu, masomo ya form 1 tz ndio hayo ya msingi kilichobadilika ni lugha tu
 
Sometimes tunaexagrate uwezo wa wanafunzi toka kenya .kuna advantage ya kiingereza tu. Sasa wazazi wengi wana hangover ya mkoloni kudhani kiingereza ndio elimu . Chukua mtoto anayesoma physics au maths ngazi ya form six au university toka kenya na tanzania utakuta elimu yao ya kusolve maswali ya somo husika wako sawa. Kama ingekuwa english ndio suluhisho basi malecturer na maprofessor wa university za tanzania wangekuwa waliosomea kenya na huko nje waliosomea huko mnakosifia. Kupeleka mtoto nje ni arrogance ya pesa ya matajiri tu basi, haina uhusiano na weledi wa mtoto wa masomo huko mwishoni. Ukitaka kujua ukweli huo chukua mtoto mwenye division one ya tanzania halacu mpe scholarship aende chuo bora huko nje, labda marekani MIT au HAVARD ,husezi kukuta amerudishwa kwa kufeli. Kinyume chake hao wanaosomea huko sekondari za kenya hata sifa za kwenda university za nje huwa wengi hawazipati. Mungu ni mwema sana, hatima ya mtoto kimasomo inategemea IQ yake na bidii ya kusoma. No wonder maprofessor wote ni weny background ya wazazi wenye kipato cha kawaida tu. Matajiri somesheni nje kuandaa watoto watoto wenu waje kuendeza biashara zenu lakini kudominate vacancy za serikali ,never on earth . Working class ndio wataendelea kudominate nyanja zote za ajira. Hata marekani na ulaya and the word over kanuni hiyo inafanya kazi. Pesa haitakuja iamue uslewa wa masomo, nawasilisha.
 
Sio kweli. Ila pia lugha na elimu ni mapacha. Nimekusoma ww unaongea nadharia mi nina evidence. Ila unaruhusiwa kubisha na kutukana maana ndicho unachoweza.
Mzee mimi nimesoma bongo nilichosoma std 6&7 ndio nilichosoma form kwa kingereza, kama kuna additional ni kiduchu
 
Uganda bora na Tz, ndio maana wanaofeli Tz form four wanaenda kuendelea form five Uganda.
Lakini kumbuka UG hawafundishi Kiswahili kwa shule za kawaida isipokuwa shule za mafunzo ya kijeshi pekee! M7 alishatia breki hio lugha kwa raia wa kawaida
 
Lakini kumbuka UG hawafundishi Kiswahili kwa shule za kawaida isipokuwa shule za mafunzo ya kijeshi pekee! M7 alishatia breki hio lugha kwa raia wa kawaida
Tatizo kuu hapa siyo lugha, kama ni kingereza Tanzania kuna English medium nyingi tu wanafundisha kingereza. Tatizo kubwa kwa elimu yetu ni mtaala kwa ujumla, mtaala wetu umechezewa sana hasa kwa miaka ya hivi karibuni.
 
Elimu sio kusolve maswali pekee.

Ni suala la connection na exposure.

Ukisoma IST sio sawa na aliesoma Kibasila.

Mitazamo ya maisha itatofautiana kwa kiasi kikubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…