Wife amanichosha nataka kumtema lakini gharama !!-sina raha ya ndoa



Ndugu story ni ndefu sana,kwa ufupi hakubali chochote ni mbishi/mgomvi balaa,kama ningekuwa ninatabia ya kupiga nadhani ningekuwa nimeua,nimekuwa najaribu kutumia technics mbalimbali maana ni muhimu kujihami asije akaleta madhara llakini sioni mwelekeo,ndo maana natafuta mtaalamu/mshauri,anishauri jinsi ya kumtoka bila kuleta madhara.
 


Unajua hadi nimefikia hatua ya kuwaza kumuacha nimejaribu mambo mengi sana,nimemkanya lakini tatizo lake ni kuwa hakubali kosa,na kuhusu kumrudisha kwao sio shida lakini inaonekana amejipanga na kunadalili ya kunisumbua that,s why natafuta technical advice kabla sijachukua uamuzi wowote.asante
 
Pole sana, nafikiri kuwa mke wa pili si jambo rahisi hata kwa huyo mwanamke. Si rahisi sana kulea watoto wa mwanamke mwenzio kama wako....ni rahisi sana kunyoosha kidole lakini ukiyaishi maisha ya mke wa pili na mama wa watoto wasio wako utaelewa. Sisemi anachofanya huyo mama ni sahihi,ila ningetamani sana kusikia mawazo yake kuhusu maisha yake na wanao....wanao wanamchukuliaje na yeye anajisikiaje na anawachukuliaje......na ikumbukwe tu,tafiti zinatuonyesha mwanamke wa pili hawezi kuwa na nafasi katika moyo wa mwanaume kama ya yule wa kwanza....men tend to compare aliyepita na wa sasa na kwa hili unakuta wana wa judge unfairly.

Sikushauri umuache,mweke chini wewe na wazee wa pande zote mbili,mwambie kuhusu mwenendo wake na unavyojisikia,mpe muda na kuwa nae karibu katika kila hatua kuhakikisha anabadilika....lakini pia washauri watoto wako na angalia mwenendo wa watoto wako kwa mama yao.....mama si malaika,kama wanamtenda visivyo ata react tu in a negative way,ila kisa ni mama wa kambo ataonekana mnyanyasaji. Karibu kwa ushauri anytime,its part of my job!
 




Mkuu nakushukuru sana ,hapa nimeshapata point tatu za muhimu sana,lakini suala la kuwapeleka watoto kwa relatives bado naona linaugumu fulani,sio kwamba sina ndugu hapana,lakini watoto wananihitaji sana na sipendi kukaa mbali nao,lakini nitafikiri na kulitathmini hilo wazo bado nina muda kwani sitaki kukurupuka,asante sana.
 




Asante kwa ushauri wako mzuri,taufanyia kazi, asante
 
kaka hazina yako pekee ni watoto,lea watoto wako wakue kwanza at least wafikie college ndipo umtafute mwenza!la sivyo watoto watachanganyikiwa.
 

aisee una moyo! Mi ningeshaua, unaishi na shetani? Bora uishi ka padre ka huwez unaweza kuoa kimila, kwani ili iitwe ndoa lazima mkale bata club jimkanaz?
 
Mkuu, Kuna kitu kinaitwa MAOMBI, watakwambia mengi ila usipo mshirikisha BWANA yote ni bure. Lazima ukaze goti. Kuna jambo lolote linalo mshinda BWANA? BWANA kwetu ni kimbilio. U must claim for HIS promises, they are meant for you. Call upon HIM and HE will show you great things!
I will always remember you in my prayers.
Otherwise I really feel extremely sorry for you and May the Good LORD Bless and keep you.
 
nashindwa nikushauri nini,kwa ujumla mimi kwangu damu nzito kuliko huyo mke mpita njia,yaani kwa hizo tabia tayari ujue kuna mambo mengine pia anakusaliti.kashaota pembe huyo.piga chini weka pengo tafuta mwanamke wa kusaidia kulea watoto na sio mke tena
 
pole kaka yangu,
mim tu sio wewe baba ya hao watoto lkn roho imeniuma sana hadi nasikia kulia kwa jinsi ulivyoelezea,
niko weak sana juu ya watoto,
lkn kaka yangu hakikisha wanao hawamdharau huyo mama,
pia watoto wakikosa muache mama awaadhibu kama mama yao,
ila pamoja na yote hatakiwi kuwatesa watoto.
Je huyu mama hajawahi kukulalamikia chochote juu ya tabia za watoto.
hali kama hizi zinakosesha sana raha.
 
.nakuonea huruma na nawaonea huruma hao watoto{napenda sana watoto}na nimepitia mambo ya mama wa kambo,kwa kweli unakuwa mnyonge na unakuwa na donge ambalo ngumu kufutika,mtetezi mkubwa kwa hao watoto ni wewe.kama una uwezo ungetafuta ndugu yako yoyote ukakaa nae,maybe itakuwa dawa kwa huyo mama,na usichoke kuwatetea watoto wako,maana hata wakiwa wakubwa,watajua wewe huna makosa yoyote yale.
 

Fanyia kazi hapo kaka!
 

Hiyo ndiyo hulka ya wanawake! Ni asili yao kupenda vyao tu. Achana nae mpumbavu huyo. Ingekuwa mimi, ningepata uchungu sana manake kwa tabia hiyo ananifanya nimkumbuke mke wangu aliyefariki. Samahani wanawake kama nimewakwaza!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…