Sheillah Sheillah
JF-Expert Member
- Jun 17, 2020
- 653
- 1,698
Mume wako anakuambia mke wangu leo tutoke tukapate hata dinner nje, wewe unajidai wife material unamwambia mtapoteza hela bora mpike nyumbani. Siku nyingine anakuambia mtoke hata mkamwagilie moyo kidogo kama kawaida wife material unakataa unamwambia ni bora mnunue mmwagilie nyumbani.
Unamwambia ni matumizi mabaya ya pesa hiyo pesa ya kwenda dinner nje ni bora sijui mfanyie hivi au vile na hiyo pesa anayotaka mkapige maji ni bora muwatumie wazazi wenu.
Ukiiangalia kwa mbali inaonekana kama wewe una akili na ni wife material ambaye mwanaume yeyote anahitaji ,ofc ni wife material, na hautampoteza mume wako ila madhara yake ni makubwa.
Wewe haufikirii labda mumeo anataka mtoke ili awe na wewe nje ya mazingira ya nyumbani akuone vile ukivaa kimtoko mtoko unapendeza ( ukizingatia wengi tukiwa nyumbani ni madera tu). Yaani wewe haufikirii kwamba mume wako anahitaji huo muda kwa ajili yenu , mbali na kelele za watoto nk?
Basi juzi rafiki yangu kaenda Bar kumfumania mume wake na mchepuko wanakunywa mapombe na makange ya kuku huku wanafurahia live band. Mume pale pale kamwambia mkewe nikikuambia tutoke out hautaki wewe endelea kuwa mama wa nyumba maana hautaki kuiacha pekee yake.
Haya endeleeni kuwagomea wanaume zenu kutoka, kule kwenye bata kuna wadada wanaovizia wababa wanaokuja pekee yao, watakula hizo hela ulizokataa kuzila wewe.