Wifi yangu amezidi

Siku zote maskin akipata ma***ko hulia mwata,
Na akunyimye kunde hukupunguzia ma***zi bibiee!
Mambo ya wakurugenzi waachie wakurugenzi!!
 
achana nae kwanza mpotezee na no yake ifute kwenye simu yako!
 
Wahenga walisema Tenda wema nenda zako dada....

sio lazima kila jambo jema tunalotendea wengine malipo yapitie kwa wenyewe kuna baraka unazipokea kupitia kwingine bila kujua.Shukuru sababu ulipata nafasi ya kufanya uliyoyafanya kwa wakati wake.


Jamani mbona wakati hana kitu alikuwa anakuja kulala kwangu leo kupanda cheo ndo iwe dharau hivi?
 

Sawa kumbuka haya ni maisha tu je na mm ningemfanyia dharau wakati anasoma Chuo si ingekuwa balaa.
Kinacho niuma kaja na bia nyumbani hata kushuka kwenye gari hakushuka akawa ananieleza hayo kibaya zaidi alikuwa na bia akawa anazitupa chini eti utakunywa hizo kashusha kioo ananitupia kama mbwa nyie mnao mtetea hayajawakuta yaani nitupiwe bia chini kwa vile mimi maskini kweli??????????
 

pole kweli anadharau sana,lakini mpotezee pesa imeonye uhalisia wake.hapo mwanzo alikuwa anapretend tu.haya ni maisha kuna kupanda na kushuka,uyo asimsubiri ashuke we mpandie huko huko ili mdharauliane vizuri.
 

Hahahahahaaha.
Haya bwana malizaneni wenyewe maana hii kesi mi siiwezi.

Ila kabla sijaaga. . . kama amekukera sana mweleze kwa text au simu badala ya kulalamika hapa wakati mwenyewe hajui kwamba umekereka.
 
Please mtoa mada
kwanza huu ni uswahili, ukimsaidia mtu akiwa chini fanya sababu unataka fanya sio deni ili akulipe for a life time.

Sasa mie niliyesoma kwa kuchangisha kijiji ntalipa wangapi?

Afu jaribu kupitia kipengele cha CEO na tabia zao na sehemu wanazopaswa kuishi.
 
Jamani mbona wakati hana kitu alikuwa anakuja kulala kwangu leo kupanda cheo ndo iwe dharau hivi?

Hii sio dharau wala nini. Julieth wacha nikupe nondo kidogo tu. Ukiwa mkurugenzi ujue shirika unalofanyia kazi linakulinda kama rasimali mtu wa juu (VIP) utapewa marupurupu mengine tofauti na mameneja wote. Ukisafiri unalipwa usafiri wa 1st Class .Malazi unalipwa fedha ya first class na utatakiwa ufanye hivyo yaani usafiri na ulale sehemu ya hadhi yako.

Kwa ufupi ukienda kinyume chake unaweza poteza hata huo ukurugenzi maana kama umelipwa 100,000 malazi halafu ukalale guest ya 30,000 wewe ni mwizi au mbadhifilifu. SEMBUSE akalale huko kitaani kwenye vyoo vya passport?

mwenye thread hajaui haya labda. Next time ajifunze maana kama akibahatika kuukwa ukurugenzi kama wifi yake , hakika atafanya hivyo hivyo . Wale kule Bungeni wanaolala guest mshezi wamezoea wizi , usijilinganishe nao bana.
 
Au anakulipa uliyomfanyia alipokuwa anakaa kwako??Labda ulimnyanyasa....
 
Jamani mbona wakati hana kitu alikuwa anakuja kulala kwangu leo kupanda cheo ndo iwe dharau hivi?

Sio dharau, mwache atumie "privilege" zake. Hata mimi nikisafiri sipendi kufikia kwa ndugu, jamaa na marafiki, huwa napenda nifikie Hoteli kila nnapoweza, yanini tabu na raha ipo. Wakati hana, mtabanana hapohapo, lakini anaweza kwa sasa, kheee, mbona mna nongwa hivi?
 
Reactions: BPM
Inawezekana kielimu she wasn't deserved the position of being mkurugenzi, lakini Makalio yakampa qualification!

Mungi taratibu
anakutana na wakurugenzi wenzie kwa vikao vya jioni
 
Kimeniuma sana kitendo cha kunitupia bia za kopo kama mbwa jamani ubinadamu kazi kwakweli

Wewe nae kakutupia kakuletea? mtu yupo ndani ya gari, bize, kakushushia haraka haraka, ngoja atakualika hukohuko ndio utasema vizuri.
 
Jamani humu hamna Mkurugenzi hata mmoja aeleze kuhusu hili la mkrugenzi wifi? Duh
 
ebu bandika picha yake tumuone!
 
Wewe nae kakutupia kakuletea? mtu yupo ndani ya gari, bize, kakushushia haraka haraka, ngoja atakualika hukohuko ndio utasema vizuri.

Mtu yupo ndani ya gari bia zipo kwenye ctn alikuwa anatoa moja moja na kurusha chini kama angekuwa mstaarabu si angenipa ctn yote kuliko kutoa kopo moja na kutupa mchangani eti mtakunywa hizo mi nimetosheka
 

Kwa hiyo hata kunitupia bia chini nayo sio dharau ni privilege za wakurugenzi sio?
 
Pole dada ila all in all co tabia nzuri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…