Wachambuzi hawa wanajaribu kuibeba ionekane timu kuubwa Afrika lakini matokeo uwanjani yanawasaliti. Walisema maneno yote mabaya juu Al Hilal na wakafikia kumpa hat trick mtetemaji lakini haikusaidia.
Kwa sasa wanazidi kuwaaminisha wenzao kuwa walikuwa bora kuliko timu isiyo na muunganiko kwani imeokoteza wachezaji wenye viwango vidogo kuliko wao. Kwa hiyo wameaminishwa wanaweza kupindua meza kibabe huko Sudan.
Wanahisi ni rahisi hivyo kwa vile wao tu ndiyo wanataka kuingia makundi na wenzao ni kama hawajajipanga. Bado hawajawaheshimu tu wapinzani wao, eti kwa kuwa walisawatoa St Georges kwa faida ya goli la ugenini.
St Georges wao wanaiona kama timu dhaifu kwa vile ilifungwa na Simba goli 2. Na kibaya zaidi waliiona Al Hilal kuwa mbovu kwa kuwa iliwahi kufungwa na Simba goli 4-1. Na kwa ujinga uliopitiliza, walijisifu pale ilipofungwa goli 3 na wachezaji wa akiba wa TP Mazembe muda mfupi kabla ya mechi ya Dar.
Wachambuzi hawana raha kwa vile wanashindwa waizodoe vipi Simba. Wanajipa moyo kuwa Simba ni mbovu kwa vile Namungo alifanikiwa kuwafunga wapinzani wao goli 6. Kwa sasa wanasubiri tarehe 23 waone Simba inavyofungwa ili wapate kuisema sana kwamba ni dhaifu.
Wachambuzi wa mchongo poleni sana tunayaona maumivu yenu wazi wazi kila mnapoingia kwenye vipindi.
Nimetabiri wengi wenu mtaacha kazi kwa kuwa timu mnayoisifia itakuwa ikiwaangusha tu kimataifa. Maana hata huko Championship, kuna wababe msifikiri eti ndiyo mtapenya huko.