Wiki hii imekuwa ngumu sana kwa wachambuzi wa soka Bongo, timu yao imewachoresha sana

Cashman

JF-Expert Member
Joined
Jun 8, 2018
Posts
3,017
Reaction score
5,294
Wachambuzi hawa wanajaribu kuibeba ionekane timu kuubwa Afrika lakini matokeo uwanjani yanawasaliti. Walisema maneno yote mabaya juu Al Hilal na wakafikia kumpa hat trick mtetemaji lakini haikusaidia.

Kwa sasa wanazidi kuwaaminisha wenzao kuwa walikuwa bora kuliko timu isiyo na muunganiko kwani imeokoteza wachezaji wenye viwango vidogo kuliko wao. Kwa hiyo wameaminishwa wanaweza kupindua meza kibabe huko Sudan.

Wanahisi ni rahisi hivyo kwa vile wao tu ndiyo wanataka kuingia makundi na wenzao ni kama hawajajipanga. Bado hawajawaheshimu tu wapinzani wao, eti kwa kuwa walisawatoa St Georges kwa faida ya goli la ugenini.

St Georges wao wanaiona kama timu dhaifu kwa vile ilifungwa na Simba goli 2. Na kibaya zaidi waliiona Al Hilal kuwa mbovu kwa kuwa iliwahi kufungwa na Simba goli 4-1. Na kwa ujinga uliopitiliza, walijisifu pale ilipofungwa goli 3 na wachezaji wa akiba wa TP Mazembe muda mfupi kabla ya mechi ya Dar.

Wachambuzi hawana raha kwa vile wanashindwa waizodoe vipi Simba. Wanajipa moyo kuwa Simba ni mbovu kwa vile Namungo alifanikiwa kuwafunga wapinzani wao goli 6. Kwa sasa wanasubiri tarehe 23 waone Simba inavyofungwa ili wapate kuisema sana kwamba ni dhaifu.

Wachambuzi wa mchongo poleni sana tunayaona maumivu yenu wazi wazi kila mnapoingia kwenye vipindi.
Nimetabiri wengi wenu mtaacha kazi kwa kuwa timu mnayoisifia itakuwa ikiwaangusha tu kimataifa. Maana hata huko Championship, kuna wababe msifikiri eti ndiyo mtapenya huko.
 
Wanahisi ni rahisi hivyo kwa vile wao tu ndiyo wanataka kuingia makundi na wenzao ni kama hawajajipanga. Bado hawajawaheshimu tu wapinzani wao, eti kwa kuwa walisawatoa St Georges kwa faida ya goli la ugenini.
 
Hawajui hawajui wanajidanganya. Kabla haijafika 17/10/2022 watakua washajua kuwa wao ni utopolo
 
Baada ya matokeo ya Simba na Yanga kimataifa last weekend ,kupitia vipindi vya michezo vya radio kadhaa nchini, niliona wachambuzi wengine wanavopata shida kui bold Yanga, na kuona Simba yanaweza jirudia ya Galaxy.

Yani unaona kabisa hawana amani.
 
Aya tumekusikia kamuombe Rage radhi aliyewalaani maana unashindwa kumuwaza mkeo kitandani unabaki kukesha ukiiwaza yanga,,rubbish!
 
Mkuu nadhani kila mtu anaruhusiwa kupenda timu yoyote na kuchambua vyovyote inavotakiwa sio lazima matokeo yaendane na vile wanavochambua.( Yupo mchambuzi sky sports huwa anatabiri mechi za weekend na anakoseaga sana na hakuna anayemlalamikia)

Shida ipo kwako wataka wachambue na kuKufurahisha wewe na una uwezo pia wakutowasikiliza maana hakuna anayekulazimisha kuwasikiliza maana nao ni binadamu na wana mawazo na namna yao ya upeo.

Upumbavu tulionao vijana wengi ni kuchukia mtu akitoa maoni yake na kuonyeshwa mapenzi na timu Fulani.
Leo hii mchambuzi akijulikana ni shabiki wa Simba basi mashabiki wa Yanga watavamia Instagram kumporomoshea matusi na hata vilevile kwa upande wa Simba wanawaporomoshea matusi wachambuzi wanaoonekana ni mashabiki wa Yanga .

Nadhani tujifunze sehemu sahihi ya kulalamika na kupeleka chuki zetu.
 
Kati ya wavhambuzi woteeee hapo mtoe Jemedari, Ibrahim Maestro hao jamaa usiwaweke ktk.uchambuzi mchwara + na Edger Kibwana ...na Lwambano ..ila kuna mwana anaitwa chukuchuku huyo ndio alikuwa wa kwanza kuamini yanga watampiga Al hilal na simba kupoteza kule angola ila ikawa vice versa
 
Siri ya wachambuzi hawa uchwara iko mkwenye mithali ya kiswahili isemayo "mtumikie kafiri upate mradi wako"!! Kisa ni bahasha za GSM!! We sifia yanga mwisho wa siku bahasha ingie kibindoni! Wanachambulia tumboni kwa taarifa yako! Wewe timu yenye nusu point (0.5) kwenye msimamo wa CAF utaipaje nafasi kwa mfano!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…