Wiki ijayo itajulikana kama Magoma alishinda kesi kihalali ama alifanya uhuni, saini ya mama Fatma Karume aliitoa wapi!

Wiki ijayo itajulikana kama Magoma alishinda kesi kihalali ama alifanya uhuni, saini ya mama Fatma Karume aliitoa wapi!

Majok majok

JF-Expert Member
Joined
Aug 3, 2023
Posts
783
Reaction score
2,057
Kuna upuuzi mwingine ni wa viwango vya lami, mahakama pamoja na weledi wake ilishindwa kunusa hali yoyote ya uhuni kwa awa wakina magoma na mwenzake? Wajumbe wa Baraza la wadhamini aliowashtaki magoma kipindi kile ni watu maarufu na wanajulikana ata makazi yao walipo na ata ofisi zao walishindwaje kuwapa taarifa za mashtaka?

Laiti Kama wangepewa taarifa izo pia wangewasilisha jambo ilo klabuni likajulikana! Jambo la kushangaza linaloonesha kesi hii ilikuwa ya mchongo Magoma alipataje saini za baadhi ya wajumbe wa Baraza la wadhamini wakina mama Fatima Karume mpaka akaenda nazo mahakamani kuonesha wamekubali washtakiwe?

Mama wa watu amebaki amepigwa na butwaa alipoambiwa kuna saini yake kule mahakamani kwenye kesi ambayo aijui Wala ajawai kuisikia? Tukirudi kwenye hoja ya magoma kudai kwamba katiba ya yanga ni batili ni hoja ya kipumbavu kwakuwa aiwezekani katiba iliyopitishwa na taasisi zote zinazosimamia mpira wa Tanzania na duniani(TFF na FIFA, BMT na RITA) iwe batili!

Mahakama kwakuwa ilisikiliza kesi upande mmoja ulioghushi kila kitu kimya kimya nafikiri ndio maana magoma alifanikiwa njama zake, but kwakuwa mahakama imekubali yanga waifanyie review na kupitia mlolongo mzima wa kesi mhuni magoma na mwenzake pamoja na yule aliyepo nyuma yake wameshaferi misheni yao mapema sana!

Yanga watawasilisha uthibitisho wao wa uhalali wa katiba yao iliyopitishwa na vyombo vyote vyenye mamlaka ya kusimamia mpira, na pia magoma na wenzake watatakiwa waseme saini ya wajumbe wa Baraza la wadhamini walizitoa wapi!

Uyo Abeid Abeid aliyesimama kama mwakilishi wa wajumbe wa Baraza la wadhamini na yeye atatakiwa aseme alitumwa na nani!

Hili suala ni jepesi kama unyoya na Engineer anaendelea kupiga kazi Kama kawaida maana kesi aimuhusu na yupo kihalali kwa katiba halali ivyo dawa ya uhuni ni kumalizana kihuni na wahuni wiki ijayo Kila kitu kitajulikana!

Soma=> Simon Patrick: Yanga itaenda mahakamani kuweka zuio la kukabidhi timu kwa wazee walioishtaki
 
Kama kweli alichokuwa anaongea mwanasheria wa Yanga, nadhan mzee atarudi kuomba radhi, yale makeke yake yote yatageuka vilio, na wanaomsapoti watamkimbia😀
 
FB_IMG_1721280405518.jpg
 
Back
Top Bottom