.
Ndugu yangu, wakulima hawajalipwa stahiki zao.
Lakini, tatizo hilo halituzuii kuhamasisha uwekezaji, na hasa uwekezaji wa kuendeleza kahawa yenyewe.
Tunahamasisha uwekezaji bila kufumbia macho dhuluma iliyotendeka.
Unajua kwa nini malipo ya kahawa yanakuwa magumu?
Tutafakari pamoja kwa njia ya mfano ufuatao:
Jifanye kufikiria kwamba, mwaka 2015 hali ilikuwa hivi:
1. Mfanyabiashara mwenye kituo cha mafuta ananywesha magari ya kampeni kwa bili.
2. Bili yote inaandikwa kwa jina la KDCU, KCU, BCU au kitu kama hicho.
3. Msimu wa kahawa unapofika, basi KDCU, KCU, BCU au kitu kama hicho, kinachota fedha ya wakuliam ili kulipa deni la kampeni za uchaguzi uliopita.
4. Fedha zinazobaki ndio zinapelekwa kwa wakulima.
5. Hoja inajengwa kwamba soko la kahawa mwaka huu limedorora.
Katika mazingira haya, mbunge aliyeingia Bungeni kwa sababu ya mchongo huu, hana uwezo wa kupiga kelele juu ya bei nzuri kwa ajili ya kahawa ya wananchi wake.
Hivyo, dawa ya ugonjwa huu sio kuzuia uwekezaji unaopigiwa debe.
Badala yake, tunapaswa kuhimiza uwekezaji huo sambamba na kuweka bayana ukweli juu ya madudu haya yaliyotendeka huko nyuma ili huko mbeleni tuendako wote waliotenda madudu haya wasikanyage mjengoni tena. C