Uchaguzi 2020 Wiki ya lala salama Tume mna sababu zote za kutupa raha

Uchaguzi 2020 Wiki ya lala salama Tume mna sababu zote za kutupa raha

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Muda unayoyoma wiki ya lala salama ndiyo hiyo tunaianza.

Kwa hakika hatima yetu kama taifa ni dhahiri kabisa kuwa ipo mikononi mwa tume zetu za uchaguzi yaani NEC na ZEC.

Maamuzi sahihi ya NEC na ZEC yataondoa joto lote lililopo na vyombo vya dola.

Kwa umuhimu sana wa salama yetu tume mnayo sababu kabisa ya kufanya lolote kuhakikisha tunapita salama kwenye uchaguzi huu sasa na hata baada ya uchaguzi.

Kuendesha zoezi la upigaji kura, kuhesabu kura na kutangaza matokeo kwa uwazi kama inavyokubalika na wadau wote kutatunasua na kutupa raha watanzania wote.

Kwa nini tume zisione umuhimu wa kuwa sikiliza au kuwashawishi wadau kwa hoja?

Eeh mola wetu ukawajalie viongozi wa tume zetu hekima yako ya kuona umuhimu wa mawazo jumuishi ili kutupa uchaguzi ulio huru na wa haki ambako dhahiri ndiyo inayozaa salama yetu.

Salama yetu kama taifa ni muhimu mno kuliko mtu yeyote mmoja au kundi lolote lenye maslahi au mtizamo binafsi.

Tuungane kuwapa tume mawazo ya nini kama wapiga kura tutashawishika kuwa haki imetendeka.
 
1. Vituoni ni muhimu wananchi watakaotaka wabakie vituoni kusikiliza matokeo yakitangazwa.

2. Matokeo yatangazwe vituoni mara tu baada ya kumaliza hesabu. Kuhesabu kura zisizodi 200,000 hakiwezi kuchukua masaa 2 hata kwa kutumia wanafunzi wa darasa la 3.

3. Uwazi uliowanyoa kina Pascal Mayalla kawe, silinde nk kwenye kura za maoni CCM ni desa la kutosha kwa NEC na ZEC.

4. Aliyeshinda na atangazwe na si vinginevyo.
 
1. Vituoni ni muhimu wananchi watakaotaka wabakie vituoni kusikiliza matokeo yakitangazwa.

2. Matokeo yatangazwe vituoni mara tu baada ya kumaliza hesabu. Kuhesabu kura zisizodi 200,000 hakiwezi kuchukua masaa 2 hata kwa kutumia wanafunzi wa darasa la 3..
Hawataki wanajua CCM itaenda na maji
 
Watuondolee kwanza wagombea ambao wamejivua uanachama wa vyama vyao zitto Kabwe na Maalim Seif kwa kuvunja katiba za vyama vyao
 
Kila mtu atimize wajibu wake, hakuna HAKI bila wajibu!
Hiiiii bagosha mkisikia haki ikitendeka amani itapatikana kwa nini mnakotaka hivyo?

Haupo wajibu mnakereka hivyo? Mtu kutenda haki bali kutenda haki ni wajibu wa kila mwungwana na hasa kila mpendwa amani.
 
magufuli mitano tena

Mitano tena hata kama ni ya dhuluma?

Kwa nini isiwe kwenye mazingira huru na ya haki na wengine washawishike kuwa hakukuwa na wizi?

Uwazi uliowanyoa kina Pascal Mayalla kawe, ni kigezo bora kabisa.

"Hata mwana JF yule alithibitisha uchaguzi kwenye kura za maoni CCM kuwa kwa hakika ulikuwa safi, huru na haki."

Kwanini na huu usiwe vivyo hivyo?
 
Back
Top Bottom