Uchaguzi 2020 Wiki ya Mwisho inavyoweza kumpaisha au kumdondosha Tundu Lissu

Uchaguzi 2020 Wiki ya Mwisho inavyoweza kumpaisha au kumdondosha Tundu Lissu

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Joined
Mar 27, 2012
Posts
1,761
Reaction score
2,391
Upepo ulikuwa kwao wiki iliyopita na kuonesha mvuto wao ulikuwa mkubwa sana kitaifa. Ila ni makosa madogo yanayoweza kupunguza kura zao na wakiepuka tu wanaweza kuongeza kura sana na hata kuishangaza dunia.


1. Hofu inayojengwa na CCM dhidi ya CHADEMA

Hofu hizo sio za kupuuza na kiutafiti ukiuliza Wana CCM wengi wapo huko kwaajili ya hofu hiyo.

A. Hofu kuwa wanatumiwa na wazungu ili wapore rasilimali.

Hoja hii nadhani inatokana na mgombea wao kukaa nje kwa muda mrefu. Hoja hii haijajibiwa kabisa na mgombea mwenyewe Ila watu wengine kabisa kupitia mitandao ya kijamii.

Wapo walifananisha matibabu aliyoyapata Nyerere hadi kifo Uingereza. Alipofata chakula cha msaada wMarekani 1984 (wakati wa njaa ali) na hotuba zake za kudai Uhuru UNO.

B. Hofu kuwa hawawezi kulinda Amani ya nchi

Kuitoa hofu dhidi yao kunaweza kuwaongezea mpaka asilimia 5-10 ya kura. UCHAGUZI huu hata asilimia moja ni muhimu Sana. Je, vipi wataitoa hofu hii ni kazi ngumu sana lakini lazma waifanye ili waongeze hata asilimia 3-5 za kura.

Sio busara lakini lazma watengeneze hofu kubwa dhidi ya CCM awamu hii ya Pili. Lazima waoneshe hali inaweza kuwa mbaya mara hata kumi ya ilivyo Sasa. Hiyo inaweza kuwapunguzia CCM Hadi 5% ya kura, Kwa mifano dhahiri na ushawishi mkubwa.

Ndicho anachokifanya membe. Anasema nchi haina hela na Serikali imekopa Sana mpaka haikopesheki tena. Miradi mikubwa haitakamilika yote na itatelekezwa na ata Ile midogo kama ujenzi wa soko na stendi Mwanza haijakamilika.

Ila labda angewaambia watumishi wanapoelekea sio kukosa nyongeza za mshahara na kuchelewa Pensheni tu Bali hata mshahara wenyewe wanaweza wasiupate.

Pili kuweka mikakati wa kuwaokoa wapiga kura waliokata tamaa. Wapo wapiga kura wengi Sana huwa na manung'uniko mengi na wamekata tamaa kabisa kupiga kura.
Huona siasa NI Uongo na ahadi zote huwa NI hewa. Kwa utafiti mdogo niliufanya mwaka huu karibu 35 asilimia uwenda wasipige kura kwa sababu tofauti. Na Kati yao Hadi 20% wakiwekewa mkakati wanaweza kupiga kura. Hawa wasiopiga kura NI hazina kubwa ya upinzani.

Hawa wakishawishiwa na kuimizwa, wanachama na washabiki kuimizana kwenda tu kupiga kura bali na kila mwenye Nia kupitia watu wawili na kuhakikisha kupitiana na kwenda kwa makundi kupiga kura. Kati ya hizo asilimia 20, 15 wananafasi kubwa ya kupigia upinzani. Na hivyo kujiongezea Hadi 10% asilimia zaidi ya CCM. Na kuwashawishi sio Kazi rahisi.

Na mwisho kuiua hoja ya upinzani upo kwaajili ya kupiga kelele tu na sio kuongoza.

Chadema wasipofanyia Kazi hivyo vitu Muhimu basi wasije wakashangaa matokeo vituoni yakawa tofauti kabisa na matarajio yao.
 
Nimekumbuka UKAWA siku ile ya mwisho wa kampeni pale JANGWANI na Tshirt yangu imeandikwa MALOFA dah ! Safari hii nimekuwa busy kwa mambo yangu binafsi zaidi . Nadhani nimeshakuwa mkubwa sasa 😂😂😂😂😂😂
 
Upepo ulikuwa kwao wiki iliyopita na kuonesha mvuto wao ulikuwa mkubwa sana kitaifa. Ila ni makosa madogo yanayoweza kupunguza kura zao na wakiepuka tu wanaweza kuongeza kura sana na hata kuishangaza dunia...

Huu mwaka CCM kupitia kile kijamaa kinaitwa Polepole sijui , mmeamua kuongea ukweli toka mioyoni kwa kukubali kuwa nyie hampo kwa ajili ya wananchi maskini.

Kamwe hamjawahi kuwa. Zaidi ni kwamba mnastahili kuondoka madarani. Mmekula mmevimbiwa, hamna UTU. Hadharani mnawatweza walalahoi walipakodi mnazofuja!
 
Upepo ulikuwa kwao wiki iliyopita na kuonesha mvuto wao ulikuwa mkubwa sana kitaifa. Ila ni makosa madogo yanayoweza kupunguza kura zao na wakiepuka tu wanaweza kuongeza kura sana na hata kuishangaza dunia...

Huna ushauri mbaya, Ila Nataka kujua, umewahi kusikiliza hotuba zote za kampeni za Lisu, au unasikiliza viclip vifupi fupi huku mitandaoni, na sehemu ndogo sana kwenye media rasmi? Maana unavyoviona huku ni sehemu tu ya anachosema, na vinaletwa na watu kwa utashi wao.
 
Ameshalegea!!
Acheni Mzee Apumzike Mtamuua Kwa Pressure
 
Hizo siyo hofu za wananchi bali ni propaganda nyepesi za CCM ambayo haina tena ushawishi kwa Wananchi.
 
1) Hakuna wezi walioiibia Nchi hii rasilimali zake isipokuwa viongozi wa nchi waliotoka CCM. Nipe mfano wa mpinzani mmoja aliyeshitakiwa kwa ufisadi. Hoja ya uizi wa rasilimali za nchi inapaswa ijibiwe na CCM.

2) Kukaa kwa Lissu ulaya ilikuwa ni kwa matibabu ya majeraha makubwa aliyosababishiwa na shambulio ambalo ama watawala walilipanga au wanajua aliyehusika.

3) kama kukaaa ulaya kwa miaka 3 ndio hoja ya ku-conspire na wazungu, Tusemeje kuhusu Kikwete aliyetumia takribani nusu ya utawala wake akisafiri kwenda huko kwa hao wazungu.

CCM inachofanya kwa sasa ni propaganda za kihuni na hazitafanikiwa. Maana upinzani haujaletwa na Lissu Bali ni uelewa wa watz HIV sasa umekuwa na wanajitambua.
 
Kipindi cha kampeni kikiongezwa mwezi mzima Lussu hawezi kurudisha kura alizozipoteza kupitia shehe Ponda.
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani nidhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.
 
Hii Nchi ime ongozwa / kutawaliwa na CCM toka Uhuru ,Mikataba yote mibovu na isiyokuwa na tija juu ya Raslimali zetu imesimamiwa na Watendaji wa Serikali ambao kimsingi wanatokana na CCM.

Hayo mengine ni Hisia zako tu unaamua kuziweka huku kwa kuzi jenge hoja dhaifu kabisa ,Lissu akishika Madaraka leo atakuwa amerithi Madudu yote yaliyo kwisha kufanywa na wana CCM.

2594490_images.jpg
 
Uchaguzi huu CCM inakwenda kushinda kwa kishindo kwakua upinzani ni dhaifu kuliko wakati wowote tangu kuanzishwa kwa vyama vingi.

Mtahangaika sana safari hii ,lakini lazima mtage.
 
1) Hakuna wezi walioiibia Nchi hii rasilimali zake isipokuwa viongozi wa nchi waliotoka CCM. Nipe mfano wa mpinzani mmoja aliyeshitakiwa kwa ufisadi. Hoja ya uizi wa rasilimali za nchi inapaswa ijibiwe na CCM...
Watanzania elimu yetu ni ya kawaida sana. Kila hoja lzm ifafanuliwe kwa Lugha nzuri na nyepesi ili ieleweke
 
Back
Top Bottom