Wiki ya nne hii nakohoa nameza dawa siponi

kimsboy

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2016
Posts
9,846
Reaction score
20,319
Habari waungwana wa jukwaa hili
Nimeanza kukohoa ni wiki ya nne hii
Mwanzo hali ilikua mbaya sana nilikua nakohoa mpaka nakosa usingizi hususani wakati wa usiku
Nilikua nakohoa sana mpaka koo likawa linaniuma nilimuona daktari nikamweleza akanipa dawa nikapata nafuu kidogo nikawa at least limepungua nikawa napata usingizi
Sasa hivi nimeanza kukohoa tena hususan jioni ikiingia
Nimejaribu kutumia mpaka dawa za minyoo lakini sioni change yoyote
Naombeni mnishauri wakuu
 
Pole sana mkuu..ngoja tuwasubiri wataalamu wa afya bila shaka utapata tiba!

young kilimanjaro
 
Pneumonia, tb , minyoo inayofanya heart lung migration..

All in all kamuone dr aliye karibu na wewe ili akuchukue history vizuri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Acha kunywa dawa wewe, jiulize kwa nini unakohoa, mimi niliisha kohoa kama miezi miwili n a zaidi mtu anaweza dhani ni TB, kumbe mimi nilikuwa nabomoa banda la bati yenye kutu na vumbi ndo nikapata hicho kifua. nilikohoa balaa.
 
Utachukulia kama utani ila amini usiamini hakuna dawa ya kikohozi kama uji uliowekewa asali Fanya angalau kutwa Mara mbili siku mbili nyingi

blame no body
 
Unatumia dawa gani.?

Si uende upime?,

japo mimi nikipata kikohozi kisipoisha ndani ya wiki nakunywa amoxline mbili mara tatu kwa mda wa week nzima,napona ndani ya siku mbili ,japo ukipona maliza dose usiishie njiani
 
Unatumia dawa gani.?

Si uende upime?,

japo mimi nikipata kikohozi kisipoisha ndani ya wiki nakunywa amoxline mbili mara tatu kwa mda wa week nzima,napona ndani ya siku mbili ,japo ukipona maliza dose usiishie njiani
 
Mkuu kunywa tangawizi ile ambayo ni kali sana usipopona njoo unishudie uongo
 
rudi hospitali na omba upime tb usiende dispensari nends hospitali mkuu
 
Tumempoteza kijana angali mdogo Hii ni Dalili ya UKIMWI pia cha Ajabu member wengi hawajakushauri go and take HIV test
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…