Wiki ya Unyonyeshaji 2024

Wiki ya Unyonyeshaji 2024

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Wiki ya Unyonyeshaji Duniani hufanyika katika wiki ya kwanza ya Agosti kila mwaka, (Agosti 1-7)

Kaulimbiu ya mwaka 2024 ni Kuziba Pengo: Msaada wa Unyonyeshaji kwa Wote, ikilenga kuwaandimisha Wakina Mama wanaonyonyesha, huku ikionyesha jinsi familia, jamii, na wahudumu wa afya wanavyoweza kuwasaidia katika kurahisisha Mchakato wa Kunyonyesha

Kwa mujibu wa Sheria ya Ajira na Mahusiano Kazini ya Mwaka 2004 na kanuni zake za Mwaka 2017, Mwanamke aliyejifungua ana haki ya kupewa likizo ya uzazi yenye malipo ya siku 84 akijifungua mtoto mmoja, na siku 100 kama atajifungua watoto mapacha

Pia akirudi kazini ana haki ya kupata ruhusa ya masaa mawili kwa siku kwa ajili ya kumnyonyesha mtoto. Ruhusa hiyo ya masaa mawili atakubaliana na mwajiri muda unaomfaa


.......

World Breastfeeding Week is held in the first week of August every year, supported by WHO, UNICEF and many Ministries of Health and civil society partners.

The theme for 2024 is Closing the gap: Breastfeeding support for all.

The campaign will celebrate breastfeeding mums in all their diversity, throughout their breastfeeding journeys, while showcasing the ways families, societies, communities and health workers can have the back of every breastfeeding mum.

Source: WHO
 
Sema uzazi zamani kidogo uliheshimika sana maeneo ya kule kwetu mama akijufungua ile tu amerudi home kama ni mtoto wa kike vinapigwa vigelegele(Midoro🤗) vinne kwa mtoto wa kiume ni Vitatu 3️⃣ lakini kubwa kuliko ni kwamba vyakula vinavyopikwa iyo nyumba ni vile vilivyoeenda shule 😋, kwanzia masupu, uji wa Ulezi, vitu nyama nyama ndio zinakuwa nyingi basi na watoto wa jirani tunasogea pale kucheza cheza(akili mtu wangu) hapo katikati(along the way) lazima Atachinjwa mnyama(Kondoo) anachinjiwa mama hii ina maana yake ukiweza kuelewa hii 👉🏾 “Urushu Mboria mboriaakindo lulema ivyara”😂😂 ukifungua iyo code vocha ya buku ipo, yote 9 10 vyote hivyo hufanyika kuhamasisha UNYONYESHAJI na Afya ya Akili,
 
Back
Top Bottom